Mkurugenzi
Mkuu wa mfuko wa PPF Bw. William Erio (kushoto) akipokea michoro ya
jengo jipya la PPF Jijini Arusha kutoka kwa Mbunifu na Msimamizi Mkuu wa
mradi wa ujenzi wa jengo hilo, Bw. Dudley Mawalla (kulia) kutoka
kampuni ya MD Consultancy Ltd ya Dar es Salaam, katika hafla fupi ya
makabidhiano rasmi ya jengo kutoka kwa mkadarasi wa kichina CREJ (EA)
Ltd. Anayeshuhudia Katikati ni Injinia wa Miradi ya PPF, Injinia Marko
Kapinga.
DG
William Erio (pichani juu) ameisifu timu yote iliyoshiriki kufanikisha
kukamilika kwa mradi huo katika ubora uliotakiwa na katika bajeti
iliyopangwa mwaka 2012 bila kuongezeka pesa yoyote, kuanzia kitengo cha
miradi ya PPF makao makuu, wabunifu na wasimamizi, mamlaka za Jiji,
idara nyingine za Serikali na wakandarasi wenyewe.
Jengo
hilo maalumu kwa shughuli za ofisi na biashara lenye ghorofa 10
sambamba na eneo la basmenet yenye uwezo wa kupaki magari 168, lina
thamani ya shilingi bilioni 32.5. Limejengwa eneo la Corridor, Kitalu
Na. 15 Barabara ya zamani ya Old Moshi Jijini Arusha. lina huduma zote
muhimu kwa majengo ya kisasa zikiwemo 'lifti' za kutosha, majenereta
makubwa, mataki ya maji na mafuta ya jenerato, mfumo wa kukabiliana na
moto na bila kusahau camera 90 za usalama na eneo kubwa la kuegesha
magari ndani ya jengo.
Kwa
mujibu wa Mbunifu na Msimamizi Mkuu wa mradi huo wa kisasa, Arch
Mawala, ujenzi wa jengo hilo ulianza rasmi Agosti 2 mwaka 2018
ukitarajiwa kukamilika miezi 104 baadae na ulikamilika rasmi (practica
completion) mwishoni mwa mwezi Disemba mwakaa jana. Hata hivyo
imewachukua miaka miwili na miezi 3 kuweza kukamilisha kila kitu katika
ubora wa kiwango cha juu, ambapo miezi hiyo mitatu ni ya ngongeza ya
muda kutokana na sababu ambazo hazikuweza kuzuilika.
Sehemu ya muonekano wa mbele wa jengo
Mpaka
kufikia kukabidhiwa kwake hii leo, tayari ukaguzi wa mamlaka za Jiji na
Usalama wa Majengo umeshakamilika na ruhusa ya matumizi kutolewa.
Tayari jengo hilo limeshapata wapangaji watatu ambao wapo kwenye jengo
tayari zikiwemo benki za TIB na FBNB, huku asilimia 21 ya wapangaji
wengine wakiwa wamekwisha saini mikataba na PPF na wapangaji wengine 24
wakiwa katika mazungumzo.
Aidha kwa maelezo ya Mratibu wa PPF
Kanda ya Kasakazini, Bw Onesmo Rushahi, Ofisi za Kanda ambazo kwa sasa
ziko maeneo ya Kaloleni Jijini hapa zitahamishiwa katika Jengo hili
jipya, huku mkakati wa PPF ukiwa ni kuhakikisha baada ya mwaka mmoja
jengo hilo liwe limefanikiwa kupata wapangaji maeneo yote kwa shughuli
za ofisi na biashara.
Mkandarasi
Mkuu ni kampuni ya CRJE (EA) Ltd akisaidiwa na wakandarasi wengine kwa
huduma za jengo kama vile ICT na Usalama - SSTL Group Ltd, Lifti - S.E.C
(EA) Ltd, AC - M.A.K Enginering Co. Ltd, Mfumo wa maji safi na maji
taka - Jandu Plumbers Ltd, na Umeme ni Central Electrical International
Ltd. Pia kulikuwa na mamlaka za kiserikali kama wasimamizi wa usalama
makazini OSHA, Idara ya maji Asurha - AUWSA, NAESCO, Halmashauri ya Jiji
na Bodi za Ukaguzi kama AQRB na CRB.
Injinia
Marko Kapinga, Meneja wa Utekelezaji wa Miradi ya PPF akikagua
makabrasha yaliyokabidhiwa na mkandrasi kama michoro halisi ya namna
jengo lilivyo kwa sasa
Kiongozi
mkuu wa Kampuni ya CRJE (EA) Ltd, Bw Hu Bo (kulia) ambaye kamapuni yake
ndio ilikuwa mkandarasi mkuu wa mradi akikabidhi funguo kwa Director
General wa PPF Bw William Erio kama ishara ya makabdihiano ramsi ya
jengo la PPF Plaza la Jijini Arusha hii leo. Kwa mbali anashuhudia
Meneja wa jengo hilo kutoka PPF Bw..
Meneja
wa PPF Kanda ya Kaskazini Bw Onesmo Ruhasha (kulia) akishuhudia
makabidhiano rasmi ya jengo jipya la PPF Plaza la Jijini Arusha hii leo
Meneja
wa PPF Uwekezaji Bw Selestine Some (kushoto) akimkabidhi ufungua kama
ishara ya kuhamishia usimamizi wa jengo la PPF Plaza kwa Menenja
Rasilimali, Bw Selemani Kituli wa PPF Kanda ya Kaskazini
Msimamizi
Mkuu wa kazi zote za ujenzi kwa upande wa mkandarasi, kampuni ya CRJE,
Bw Zhang Cuishan akitoa neno la shukrani katika hafla hiyo.
Director General wa PPF Bw William Erio kulia pamoja na mkuu wa uwekezaji (PPF's Director of Investiment) Bw Steven Alfred
DG
William Erio katika picha ya pamoja mbeye ya sehemu kuu ya kuingilia
kwenye jengo akiwa na timu ya wakandarasi, wasimamizi wabunifu wa mradi
pamoja na wataalamu kutoka PPF Dar es Salaam.
Msanifu
wa jengo na msimamizi mkuu wa mradi kutoka kampuni ya MD Consultancy
Ltd, Arch Dudley Mawalla akiongoza ujumbe wa DG William Erio kufanya
ziara ya ameneo mabalimabli ya jengo kabla ya makabidhiano rasmi.
Msafara
ukitembelea eneo la kuegeshea magari chini ya jengo la PPF Plaza. Jumla
ya magari 168 yanaweza kuegeshwa katika maeneo mbalimbali yaliyotengwa
ndani ya jengo.
Msimamizi
Mradi mkaazi kwa niaba ya PPF, Injinia Norbert Nselu akitoa maelezo
kwa Bw William Erio namna gari zinavyoweza ingia basement na kuegeshwa.
Director
General William Erio akipata maelezo ya mfumo wa usalama wa kieletronic
wa jengo namna unavyofanya kazi kutoka kwa mataalamu wa maswala ya
usalama na mawasialiani ya kielectronic kutoka kampuni ya SSTL Ld, Bw
Athumani Pongwe ndani ya chumba cha usalama. Jumla ya kamera 90 za
usalama zimeunganishwa na taarifa zake kuletwa kwenye chumba hiki.
wakiangalia moja ya viambaza vya dani ya jengo.
Hapa DG William Erio na wataalamu wengine wakifurahia utani wa wake
Meeneja
wa PPF Kaskazini Bw Onesmo Ruhasha, kulia na Director General wa PPF
wakijadiliana jambo wakati wa kutembelea maeeneo ya jengo.
Baadhi
ya watumishi wa PPF Kanda ya kaskazini wakiangalia moja ya maneo ambayo
ni maalumu kwa wapangaji kufanya biashara ama kuweka ofisi za shughuli
zao.
msimamizi
mkaazi kwa niaba ya PPF, Injinia Norbert Nselu akimfafanulia DG Erio
hatua kwa hatua namna ujenzi ulivyoanza mkapa kukamilika kwake.
Director
General wa PPF akiangalia madhari ya Jiji la Arusha kutokea ghorofa ya
nane katika moja ya baraza za jengo la PPF Plaza lililokamilika na
kukabidhiwa hii leo. Pamoja nae ni Msanifu wa jengo na Msimamizi Mkuu wa
Mradi Arch. D Mawalla
Bw
Selemani Kituli (property manager wa PPF) na Bw Selestine Some, Meneja
Uwekezaji wakifahamishana jambo katika hafla fupi ya makabidhiano ya
jengo la PPF Plaza kutoka kwa Mkandarasi Mkuu CRJE (EA) Ltd
Sehemu
ya timu ya washauri wasimamizi wa mradi kwa maswala ya gharama, uimara
na huduma (Project Costs, Structural Strength na Building Services
Engineering)
Msimamizi
mradi mkaazi (Clerk of Works) kwa naiab ya PPF, Injinia Norbert Nselu
akifafanua jambo katika hafla hiyo fupi ya makabidhiano kwa Director
General wa PPF haonekani pichani.
Mkuu
wa Kampuni ya CRJE (EA) Ltd, kampuni ya kichina ambayo ndiyo ilikuwa
mkandarasi mkuu wa mradi uliokamilika wa jengo la PPF Plaza la Jijini
Arusha akitoa salamu zake katika hafla fupi ya makabidhiano ya jengo
hilo
Director
General wa PPF Bw William Erio akisalimiana na Bw Habib O Kiango, mmoja
wa watumishi wa ofisi ya PPF Kanda ya Kaskazini iliyoko Kaloleni Jijini
Arusha.
Director
General wa PPF, Bw William Erio akisalimiana na Bi Getrude Haule,
ambaye pia ni mmoja wa watumishi wa ofisi ya PPF Kanda ya Kaskazini
iliyoko Kaloleni Jijini Arusha katika hafla ya makabidhiano ya jengo
jipya la PPF Jijini hapa. Anayeshuhudia ni Bi Grace Estomih, mtumishi
pia wa PPF Kanda ya Kaskazini ofisi ya Arusha.
DG William Erio akitaniana na wafanyakazi wa taasisi anayoisimamia ofisi ya Kanda ya Kaskazini, Arusha hii leo
Director
General wa PPF, Bw William Erio akisalimiana na Bw Fortunatus Woiso,
ambaye pia ni mmoja wa watumishi wa ofisi ya PPF Kanda ya Kaskazini
iliyoko Kaloleni Jijini Arusha katika hafla ya makabidhiano ya jengo
jipya la PPF Jijini hapa.
Mbunifu/msanifu
mkuu na msimamizi mkuu wa mradi wa jengo la PPF Plaza la Jijini
Arusha, Arch. Dudley Mawalla akizungumza na wataalamu washauri wa
masuala ya gharama za ujenzi ambao walisimamia fedha zote za mradi
kwenda kwa wakandarasi na kuandaa bajeti yake, QS Mrosso (kushoto)
kutoka kampuni ya Cost Consult Ltd ya Jijini Dar es Salaam.
SHARE
No comments:
Post a Comment