Ray C amekanusha tetesi zilizoanza kuenea kuwa amerejea tena kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.
Hivi
karibuni magazeti ya udaku yamekuwa yakiripoti kuwa muimbaji huyo
amekuwa akionekana kwenye machimbo ya uuzaji wa dawa hizo jijini Dar es
Salaam.
Kupitia Instagram, Ray C ameandika maneno haya kukanusha habari za uongo:
Seriously
kwa kweli huwa naumia sana sana kuona binadam mwezangu anadiriki
kuniharibia jina langu ilj yeye apate kula!hamjui mnaniathiri kiasi gani
na hizi habari zenu?Hivi unadirikije kuandika usengwile kama huu bila
hata aibu wala picha ya kuisapoti hiyo habari yani ni ujinga ujinga tu
umeunganishwa na picha yangu bila hata uoga mmeichukua kutoka kwwnye
page yangu ya insta bassss tayari mmeshapata story ili mradi tu
mniharibie maisha yangu ili nyie mpate pesa mi nife maskini!!!kama kweli
mnauhakika na mlichoandika kwanini hamkuweka picha yangu nikivuta hayp
maunga badala yake mnaweka picha ya kituo cha mkunguni ambapo madaladala
husimamisha kituoni hapo.
Mmepiga
picha ya kituo cha mkunguni mkaona haitoshi mkaingia kwwnyw page yangu
ya insta na kuchukua picha yangu niliojipiga mwenyewe ndio mnazitumia
kunichafulia jina langu tena wakati ndio kwanza nahangaika kurudi tena
kwenye kazi yangu. Haki amungu sijawahi kuskia hata siku moja nyie
global mmeandika kuhuau foundation yangu na mambo mazuri iliofanya,jw
mnajua kama mpaka sasa nimeshatoa vijana zaid ya sabini kwenye madawa na
wako fit wanatumia methadone je mnajua hilo?
Hata
siju moja sikawahi pata msaada wowote kutoka kwenu japo kunichangia
nauli tu ya kuja kwenye dawa kila siku hakuna hata anaenisaidia huu
mwaka wa tatu bado naendelea kunywa dawa na ni kila siku ya mungu siku
saba kwa wiki hakuna sikukuu wala msiba na ukikosa mwili unauma vibaya
sana yani its not easy but am a fucking hard working woman na ni
mwanamke jasiri napambana na siogopi kujaribu,naparangana na haya madawa
na nayapinga na kamwe sintorudi nyuma na hizi nuksi mzipeleke kwenye
familia zenu.
Wewe
shigongo unamkosea sana mungu!unajifanya mlokolw lakini kazi yako ni
kuharibia maisha ya wenzio unasahau kuwa malipl ni hapahapa duniani!Mimi
ni kapuku tu sina mbwlw wala nyuma mbele yako lakini bado unanichimbia
kaburi angali mi mzima.Na wewe Mayasa Marwata ni mpuuzi usie jua kazi
yako!nimeisoma stori yako nimegundua ni mvivu Wa kufatilia habari!eti
Chimbo LA unga langu lajulikana sasa kama ushalijua mbona haukunipiga
nikivuta huo unga unaenda kupiga pixha kituo cha daladala bwege we!
Ntapambana na nyie MAHAKAMANI.
SHARE
No comments:
Post a Comment