George Simbachawene
UCHAGUZI wa mameya katika manispaa
za Kinondoni na Tameke utarudiwa, baada ya serikali kuridhia kuanzishwa kwa wilaya
mpya mbili katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Hatua hiyo inatokana na
uanzishwaji wa wilaya za Kigamboni na Ubungo.
Awali, Jiji la Dar es Salaam
lilikuwa na wilaya tatu, Kinondoni, Ilala na Temeke, lakini kwa sasa litakuwa
na wilaya tano.
Akithibitisha ongezeko hilo la wilaya,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),
George Simbachawene, alisema uamuzi huo umefikiwa baada ya Rais Dk. John
Magufuli kuridhia kuongezwa kwa wilaya hizo.
Mbali na wilaya mpya ya Kigamboni
na Ubungo, Rais Magufuli, ameridhia uanzishwaji wa wilaya nyingine tatu ambazo
ni Kibiti mkoani Pwani, Malinyi mkoani Morogoro na Tanganyika mkoani Katavi.
SHARE
No comments:
Post a Comment