Wataalam wa Upasuaji wakiangalia namna ya kufanya upasuaji kwa njia ya vitundu |
Prof. Dr Med Henning Niebuhr.Kutoka Ujerumani akitoa maelekezo juu ya namna ya kufanya upasuaji kwa njia ya vitundu |
Madaktari wakiwa kwenye Chumba cha upasuaji |
Huduma
mpya ya kitabibu imeanza kutolewa katika hospitali ya rufaa ya kanda ya
Mbeya itakayomuwezesha mgonjwa kufanyiwa upasuaji kwa njia ya vitundu
(Laparoscopic surgery) na hivyo kumuwezesha mgonjwa kupona mapema na
kuwahudumia wagonjwa wengi kwa muda mfupi.
Huduma
hiyo ambayo inatumia mashine inayofahamika kwa jina la Mnara wa
Upasuaji wa Vitundu au Laparascopic Tower inalenga kutumia muda mfupi wa
upasuaji, na kumuwezesha kufanya mgonjwa kupata naafuu mapema.
Akizungumza
na mwandishi wetu daktari bingwa wa Upasuaji katika hospitali ya Rufaa
ya kanda ya Mbeya, Dkt. Lazaro Mboma amesema kuwa mashine hiyo
itamuwezesha mgonjwa kurudi katika shughuli zake za kawaida muda mfupi
baada ya upasuaji kutokana na kutokuwa na kidonda kikubwa badala yake
mgonjwa atakuwa akiuguza vidonda vidogo vya matundu yaliyotumika wakati
wa upasuaji tu.
Pamoja
na hayo amesema kuwa kwa siku ya kwanza (leo) wagonjwa wawili waliokuwa
na matatizo ya mawe katika mfuko wa nyongo wamefanyiwa upasuaji wa
mafanikio ambapo kazi hiyo imekwenda sambamba na kuwapa mafunzo
madaktari wengine wa hospitali hiyo juu ya matumizi ya mashine hiyo.
Aidha
Dkt. Lazaro Mboma alisema kuwa mashine ya Mnara wa Upasuaji wa Vitundu
inawahusu wagonjwa wote, wale wanaotumia bima za afya na wasionazo
lakini kutokana na gharama za uendesheji inawalazimu madaktari
kuwahudumia kwanza wagonjwa wanaohudumiwa kwa bima ya afya kwani hivyo
amewashauri wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya kwani kwa mgonjwa
wa kawaida ni ngumu kumudu gharama za matibabu.
Madaktari
waliofika jijini Mbeya kwaajili ya kutoa mafunzo kwa madaktari wa
hospitali hiyo ni daktari Prof. Hening na mtaalamu wa mashine hiyo
Frolian Bets ambao wataendelea kuwepo jijini Mbeya kwa siku tatu ili
kuwawezesha madaktari wa hospitali ya Rufaa Mbeya kupata ujuzi wa
kutumia mashine hiyo.
Naye
mkuu wa idara ya upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya kanda ya Mbeya
Dkt. Mujuni Mutagwaba ametoa wito kwa wakazi wa Mbeya na mikoa ya nyanda
za juu kusini kujitokeza kutibiwa katika hospitali ya Rufaa ya kanda ya
Mbeya ili kuokoa gharama na kupata tiba stahiki.
Mashine
ya kitabibu ya Mnara wa Upasuaji wa Vitundu (Laparoscopic Tower) ni ya
kwanza mkoani Mbeya na ni vituo vichache Tanzania vilivyo na mashina ya
upasuaji ya aina hii hivyo kupelekea wagonjwa wengine kusafiri kwenda
nchi nyingine kwaajili ya kupata tiba kwa njia hii.
SHARE
No comments:
Post a Comment