Dk.Stanslaus
Ntiyakunze (aliyenyoosha mkono) akiwaonyesha mawaziri namna jengo
linavyokarabatiwa ikiwemo miundombinu yake inavyotakiwa kuwa pindi
litakapokamilika ikiwemo suala la mfumo wa maji safi na maji taka.
Kuliwa kwake ni Naibu Waziri wa Afya Dk Hamisi Kigwangalla wengine Kaimu
Mkurugenzi wa hospitali hiyo ya Muhimbili, Prof. Laurance Masaru
(kushoto) na Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu (katikati).
Mawaziri
wa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli
wameendelea kufanya kile ambacho wananchi wanataka ikiwemo suala la
kutumikia wananchi ambapo mapema leo, Februari 17, Mawaziri wa Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu na
Naibu wake, Dk. Hamisi Kigwangalla wameweza kutembelea Hospitali ya
Taifa Muhimbili kwa lengo la kukagua majengo likiwemo lile aliloagiza
Rais kuwa litumike kuwa wodi ya akina mama.
Mawaziri
hao wamefika Hospitali hiyo ya Taifa majira ya mchana na kisha
kupokelewa na wenyeji wao akiwemo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Prof.
Laurance Masaru na kisha kukagua moja ya majengo lililopo jengo la
watoto ilikuona namna ya kuweza kupunguza msongamano wa wagonjwa katika
Hospitali hyo ya Taifa.
Mbali
na kukagua majengo pia walipata kuwatembelea wagonjwa na kuwafariji
ikiwemo wodi maalum ya wagonjwa wa figo, wodi ya akina mama, wodi ya
watoto na upasuaji mdogo pamoja na wodi ya watoto wa ugonjwa wa moyo na
ile ya watoto wa ugonjwa wa kansa.
Aidha,
Waziri Ummy Mwalimu ameeleza kuwa jengo ambalo Rais ameliagiza litumike
kama wodi ya akina mama, amebainisha kuwa agizo hilo wameweza
kulitekeleza ndani ya siku moja na awali wamefanikiwa kulaza wagonjwa
zaidi ya 40 na hadi kufikia leo wameweza kufikisha wagonjwa 53.
Hata
hivyo, Waziri Ummy Mwalimu amewataka wananchi na vyombo vya habari kuwa
wavumilivu kwa kipindi cha sasa kwani tayari ukarabati unaendelea
kuakikisha miundombinu inawekwa sawa na ndani ya wiki moja itakuwa
imekamilika.
Imeandaliwa na Andrew Chale, modewjiblog
Mkurugenzi
wa ufundi, Gaudence Aksante akiwaongoza Mawaziri wa Wizara ya Afya
kuelekea katika jengo hilo linalofanyiwa ukarabati ililitumike kwa
matumizi zaidi ya wagonjwa kuondoa msongamano hospitali hiyo ya
Muhimbili.
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akipata kuwafariji watoto wanaopatiwa matibabu katika wodi maalum ya matibabu ya kansa.
Waziri
wa Afya akimjulia hali mmoja wa wagonjwa wanaopatiwa matibabu katika
kitengo cha magonjwa maalum ikiwemo Figo. Mgonjwa huyo alipongeza
mawaziri hao kwa kuweza kufika hospitalini hapo na kuwajulia hali.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati alipotembelea katika wodi ya wagonjwa wa Figo.
Waziri
Ummy Mwalimu akiwa pamoja na watoto wanaopatiwa matibabu ya ugonjwa wa
kansa katika hospitali hiyo ya Muhimbili katika jengo la Watoto.
Naibu
Waziri wa Afya Dk. Hamisi Kigwangalla akiagana na Muuguzi mkuu Bi.
Praxeda Chenya, wengine ni Waziri Ummy Mwalimu wakati wakiondoka katika
jengo hilo la watoto mapema leo Februari 17, 2016.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Laurance Masaru akitoa maelezo
namna ya walivyojipanga kuhakikisha wanasaidia wagonjwa wote wanaofika
kutibiwa hospitalini hapo. wanaofuata ni Naibu Waziri wa Afya, Dk.
Kigwangalla na Waziri Ummy Mwalimu pamoja na watendaji wa hospitali hiyo
mchana wa leo Februari 17.
SHARE
No comments:
Post a Comment