1.MTUNGI WA MAJI(WATER)
Mtungi huu una rangi NYEKUNDU wote. Mtungi huu hautumiki kuzimia moto wa umeme
au mafuta, ila unazima aina nyingine zote za moto. Mtungi huu ni hatari sana
kuutumia kwenye moto wa umeme
2. MTUNGI WA KABONDAYOKSAIDI(CO2)
Mtungi huu hutumika kuzima aina nyingi za moto ukiwamo umeme. Ni mwekundu
lakini una lebo NYEUSI kama kitambulisho chake. Wakati wa kuzima moto usishike
mwishoni mwa bomba kwakuwa gesi inayotoka ni ya
baridi sana unaweza kuganda.
3. MTUNGI WA POVU(FOAM)
Mtungi huu una rangi ya KRIMU kama kitambulisho
chake. kwingine kote ni mwekundu. Unazima moto wa vitu vya majimaji pamoja na
vitu vigumu
4. MTUNGI WA PODA(POWDER)
Mtungi huu una lebo ya BLUU kama kitambulisho
chake. Unaweza kuzima moto wa gesi, majimaji, na vitu vigumu.
SHARE
No comments:
Post a Comment