TRA

TRA

Wednesday, March 30, 2016

Mabasi ya haraka yakianza kazi Dar zile Daladala barabara ya pembeni vipi?

No comments:

Mabasi ya mwendo wa haraka kwenye jiji la Dar es salaam yapo kwenye majaribio ya kuanza kazi hivi karibuni na inawezekana ulijiuliza kama itakuwa ni chaguo lako upande Mabasi hayo au daladala barabara ya pembeni, yaani kutakua na daladala zinazofanya kazi kwenda na kutoka town japokuwa mabasi ya haraka yameanza kazi?
Taarifa ikufikie kwamba mabasi hayo yatakapoanza daladala zote zitatoka na alielithibitisha hilo March 29 2016 ni meneja mawasiliano wa mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA)  David Mziray wakati akijibu swali la mwandishi wa habari kuhusu kukosekana vituo kwenye barabara ya Morogoro.
>>>’huu mradi wa mabasi yaendayo haraka utakapoanza mabasi ya daladala yote yatatoka,  ndio maana utaona mabasi mengi yanayotumia barabara hizi za mchanganganyiko kwa maana magari ya kawaida na mabasi, hakuna vituo vya daladala kwa kuwa hiki ni kipindi cha mpito, yakishaanza haya mabasi ya mwendo wa haraka, huduma hizi za mabasi ya kawaida zitasimama’
David Mziray pia ameeleza taarifa ya kukamatwa kwa magari zaidi ya 100 ndani ya siku nne kutokana na kuvunja sheria ikiwemo kupandisha gharama za nauli za daladala na ukatishaji wa safari >>> ‘Kati ya hayo magari 105, 36 yameshafikishwa Mahakamani kwa ajili ya kusomewa mashtaka na kuweza kujibu tuhuma wanazokabiliwa na wakibainika wana makosa kutakuwa na faini, kupelekwa jela au vyote viwili’

Magazeti ya leo

No comments:
20160330_075753
20160330_075806
20160330_075817
20160330_075831
20160330_075844
20160330_075853
20160330_075909
20160330_075918
20160330_075933
20160330_075949
20160330_080006
20160330_080015
20160330_080045
20160330_080053
20160330_080112
20160330_080140
20160330_080146
20160330_080158
20160330_080205
20160330_080225
20160330_080239
20160330_080252
20160330_080259
20160330_080308
20160330_080317
20160330_080355
20160330_080401
20160330_080412
20160330_080418
20160330_080451
20160330_080538
20160330_080546

SUMATRA KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI, WAFANIKIWA KUKAMATA MABASI 105

No comments:

3
Meneja Mawasiliano wa  Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) bw. David Mziray  akiwaeleza waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu kukamatwa kwa mabasi yaliyobainika kukiuka masharti ya Leseni  nyakati za asubuhi na jioni katika jiji la Dar es salaam.Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari MAELEZO bw. Frank Mvungi.

4
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano  wa  Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) na vyombo vya habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam ukilenga kuhamasisha wadau wa Sekta hiyo kuzingatia Sheria na Kanuni zinazosimamia Sekta hiyo. (Picha na Maelezo)
Frank Mvungi-Maelezo
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi,Kikosi cha Usalama Barabarani wamefanya ukaguzi katika Jiji la Dar es salaam,ambapo wamefanikiwa kukamata mabasi  105 na kati hayo 36 yamefikishwa mahakamani  baada ya  kukiuka wa masharti ya leseni ya usafirishaji abiria.
Hayo yamwebainishwa leo  na Meneja Mawasiliano wa SUMATRA Bw. David Mziray wakati wa mkutano na vyombo vya habari uliolenga kutoa ufafanuzi kuhusu hatua zinazochukuliwa na Mamlaka hiyo katika kutatua kero zinazowakabili abiria nyakati za asubuhi na Jioni.
Akifafanua Mziray amesema kati ya Machi 21-24 , 2016  ilifanya ukaguzi huo  na ili sheria iweze kuchukua mkondo wake Kwa wale wanaokwenda kinyume na taratibu zilizowekwa.
“Katika kuimarisha huduma za usafiri Mamlaka  imeweka utaratibu maalum wa kufanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam ikiwemo katikati ya jiji,Ubungo,Buguruni na Kariakoo ili kubaini wale wote wanaovunja sheria”.alisisistiza Mziray.
Akizungumzia baadhi ya makosa yalibainika kutendwa na mabasi hayo Mziray alisema kuwa ni pamoja na kuongeza nauli,kukata njia,kutoa huduma bila leseni ya usafirishaji,kutoa huduma katika njia ambazo hawakupangiwa.
Wamiliki na wafanyakazi katika sekta ya usafirishaji kote nchini  hasa wa mabasi ya daladala wametakiwa kuzingatia sheria na kanuni za usafirishaji wanapotoa huduma hiyo kwa umma.
Mziray  aliongeza kwamba  wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa pale wanapobaini  basi walilopanda linakiuka masharti ya leseni ikiwemo kuongeza nauli,kukata njia,kutoa huduma bila leseni ya usafirishaji na kutoa huduma katika njia ambazo hawakupangiwa ambapo wananchi wanaweza kutoa taarifa kupitia namba za simu za bure ambazo ni 0800110019 na 0800110020.(P.T)

EgyptAir: Mtekaji ataka kumuona ''mkewe''

No comments:

Ndege ya EgyptAir
Ripoti zinasema kuwa mtekaji wa ndege ya EgyptAir anataka kuongea na mkewe walietengana naye anayeishi Cyprus ambaye kwa sasa anadaiwa kuelekea katika uwanja huo wa ndege.
Rais wa Cyprus Nicos Anastasiades amewaambia waandishi wa habari kwamba tukio hilo la utekaji nyara halikuwa la kigaidi,''tunafanya juhudi kuhakikisha kuwa kila mtu anawachiliwa akiwa salama'',aliongezea.
Akijibu maswali ya waandishi iwapo mtekaji huyo alishinikizwa na mapenzi,alicheka na kusema,''kila mara kuna mwanamke anayehusishwa''.
Shirika la habari la Cyprus CYBC linasema kuwa mtekaji huyo huenda alikuwa na malengo yake ya kibinafsi ,mtekaji huyo alikuwa na mkewe waliyetengana nchini Cyprus ,lilisema CYBC.
Walioshuhudia wanasema kuwa mtekaji huyo alirusha barua katika uwanja huo wa ndege ilioandikwa kiarabu akiomba ipelekwe kwa mwanamke huyo.
Ndege ya EgyptAir
Mtaalam wa maswala ya angani David Learmont ameiambia BBC kwmba rubani huyo angekataa kufuata amri ya mtekaji huyo.
''Tunaona kitu kisicho cha kawaida hapa.Rubani aliyetii amri ya mtekaji huyo kwa kuambiwa kwamba kulikuwa na mtu aliyvaa vilipuzi angekuwa na ushahidi wa kutosha kujua kwamba haingewezekana na kwamba hasingefuata amri ya mtekaji huyo." BBC

WAJUMBE WA KAMATI YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA WATEMBELEA DARAJA LA KIGAMBONI

No comments:

Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni kutoka NSSF, Mhandisi Karim Mataka akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria walipotembelea mradi wa ujenzi wa daraja hilo jijini Dar es Salaam leo.
Naibu waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde akizungumza wakati wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria walipotembelea mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara, wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mohamed Omary na kulia ni Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la hilo kutoka NSSF, Mhandisi Karim Mataka.
Meneja Miradi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo akitoa ufafanuzi juu ya ujenzi wa nyumba zinazojengwa NSSF kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria walipotembelea mradi wa nyumba za NSSF Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge wakikagua mradi wa ujenzi wa nyumba za Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) zilizopo Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam

Wajumbe wa Kamati ya Bunge wakikagua mradi wa ujenzi wa nyumba za Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) zilizopo Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam.
Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo akiwaonyesha michoro ya ujenzi wa nyumba za Mtoni Kijichi wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria walipotembelea miradi ya NSSF leo.

Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger