
Meneja
Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini
(SUMATRA) bw. David Mziray akiwaeleza waandishi wa habari leo Jijini
Dar es salaam kuhusu kukamatwa kwa mabasi yaliyobainika kukiuka masharti
ya Leseni nyakati za asubuhi na jioni katika jiji la Dar es
salaam.Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari MAELEZO bw. Frank
Mvungi.

Baadhi ya
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Mamlaka ya Udhibiti
Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) na vyombo vya habari
uliofanyika leo jijini Dar es salaam ukilenga kuhamasisha wadau wa Sekta
hiyo kuzingatia Sheria na Kanuni zinazosimamia Sekta hiyo. (Picha na
Maelezo)
Frank Mvungi-Maelezo
Mamlaka
ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kwa kushirikiana na
Jeshi la Polisi,Kikosi cha Usalama Barabarani wamefanya ukaguzi katika
Jiji la Dar es salaam,ambapo wamefanikiwa kukamata mabasi 105 na kati
hayo 36 yamefikishwa mahakamani baada ya kukiuka wa masharti ya leseni
ya usafirishaji abiria.
Hayo
yamwebainishwa leo na Meneja Mawasiliano wa SUMATRA Bw. David Mziray
wakati wa mkutano na vyombo vya habari uliolenga kutoa ufafanuzi kuhusu
hatua zinazochukuliwa na Mamlaka hiyo katika kutatua kero zinazowakabili
abiria nyakati za asubuhi na Jioni.
Akifafanua
Mziray amesema kati ya Machi 21-24 , 2016 ilifanya ukaguzi huo na ili
sheria iweze kuchukua mkondo wake Kwa wale wanaokwenda kinyume na
taratibu zilizowekwa.
“Katika
kuimarisha huduma za usafiri Mamlaka imeweka utaratibu maalum wa
kufanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam
ikiwemo katikati ya jiji,Ubungo,Buguruni na Kariakoo ili kubaini wale
wote wanaovunja sheria”.alisisistiza Mziray.
Akizungumzia
baadhi ya makosa yalibainika kutendwa na mabasi hayo Mziray alisema
kuwa ni pamoja na kuongeza nauli,kukata njia,kutoa huduma bila leseni ya
usafirishaji,kutoa huduma katika njia ambazo hawakupangiwa.
Wamiliki
na wafanyakazi katika sekta ya usafirishaji kote nchini hasa wa mabasi
ya daladala wametakiwa kuzingatia sheria na kanuni za usafirishaji
wanapotoa huduma hiyo kwa umma.
Mziray
aliongeza kwamba wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano kwa kutoa
taarifa pale wanapobaini basi walilopanda linakiuka masharti ya leseni
ikiwemo kuongeza nauli,kukata njia,kutoa huduma bila leseni ya
usafirishaji na kutoa huduma katika njia ambazo hawakupangiwa ambapo
wananchi wanaweza kutoa taarifa kupitia namba za simu za bure ambazo ni
0800110019 na 0800110020.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment