
Ndege ya EgyptAir
Ripoti
zinasema kuwa mtekaji wa ndege ya EgyptAir anataka kuongea na mkewe
walietengana naye anayeishi Cyprus ambaye kwa sasa anadaiwa kuelekea
katika uwanja huo wa ndege.
Rais wa
Cyprus Nicos Anastasiades amewaambia waandishi wa habari kwamba tukio
hilo la utekaji nyara halikuwa la kigaidi,''tunafanya juhudi kuhakikisha
kuwa kila mtu anawachiliwa akiwa salama'',aliongezea.
Akijibu
maswali ya waandishi iwapo mtekaji huyo alishinikizwa na
mapenzi,alicheka na kusema,''kila mara kuna mwanamke anayehusishwa''.
Shirika
la habari la Cyprus CYBC linasema kuwa mtekaji huyo huenda alikuwa na
malengo yake ya kibinafsi ,mtekaji huyo alikuwa na mkewe waliyetengana
nchini Cyprus ,lilisema CYBC.
Walioshuhudia
wanasema kuwa mtekaji huyo alirusha barua katika uwanja huo wa ndege
ilioandikwa kiarabu akiomba ipelekwe kwa mwanamke huyo.

Ndege ya EgyptAir
Mtaalam wa maswala ya angani David Learmont ameiambia BBC kwmba rubani huyo angekataa kufuata amri ya mtekaji huyo.
''Tunaona
kitu kisicho cha kawaida hapa.Rubani aliyetii amri ya mtekaji huyo kwa
kuambiwa kwamba kulikuwa na mtu aliyvaa vilipuzi angekuwa na ushahidi wa
kutosha kujua kwamba haingewezekana na kwamba hasingefuata amri ya
mtekaji huyo." BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment