Na Zuhura Mtatifikolo, Bunge
Katibu
wa Bunge Tanzania Dkt Thomas Kashililah leo amekutana na kufanya
mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israeli (KNESSET) Ronen Plot
aliyemtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam akitokea Nchini Zambia
alikokuwa akishiliki Mkutano wa 134 wa umoja wa Mabunge Duniani (IPU)
uliofanyika tarehe 19 hadi 23 Machi, 2016.
Akizungumzo
wakati wa kikao na Dkt. Kashililah, Mkurugenzi huyo wa Bunge la Israel,
amesema ziara yake hapa nchini kutembelea Bunge la Tanzania ina lengo
la kuwasilisha Mkataba wa Makubaliano wenye lengo la kuanzisha cha
Urafiki wa Kibunge baina ya Bunge la Tanzania na Bunge la Israel.
Plot
ambaye alimbatana na mkewe Shosh Plot, amesema Bunge la Israel
linautaratibu wa kuwa na mahusiano na mabunge mengine duniani kwa lengo
la kubadilishana uzoefu katika masuala ya uendeshaji Mabunge ambapo hadi
kufikia sasa tayari Bunge hilo lina ushirikiano wa karibu kupitia
utaratibuy huu na mabunge zaidi ya 30 Duniani kote na kwa upande wa
Afrika ni nchi Tano walizotiliana saiani na kuanzisha ushirikiano wa
namna hiyo.
Akielezea,
nia hiyo ya Bunge la Israel, Katibu wa Bunge la Tanzania Dkt Thomas
Kashililah amesema amefurahishwa sana na ujio wa Mkurugenzi wa Bunge
hilo kutembelea Bunge la Tanzania na tayari wamezingatia kwenye mipango
uanzishwaji wa Chama cha Ushirikiano wa Mabunge haya mawili kikihusisha
Wabunge kutoka pande zote mbili kubadilishana mawazo hususani katika
namna bora ya uendeshaji na usimamizi wa shughuli za kibunge.
Katika
kufanikisha hilo, Dkt. Kashililah amesema ujumbe huo utakutana na Spika
wa Bunge Mhe. Job Ndugai siku ya Jumamosi ili kufanya mazungumzo nae na
kisha kuangalia namna utekelezaji wa wazo hilo utakavyokuwa kabla ya
kutiliana saiani makubaliano hayo.
Tayari
Bunge la Tanzania lina makubaliano ya ushirikiano na vyama vya
kirafiki kutoka Mabunge mengine ya Nchi mbalimbali duniani ambazo ni
Uturuki, China, Korea Kusini, Morroco, Misri, Uholanzi na Poland
Katibu
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas
Kashililah (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel
wakati alipomtembelea leo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam na kufanya
mazungumzo naye.
Katibu
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas
Kashililah (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa
Bunge la Israel, Rone Plotwakati alipomtembelea leo ofisini kwake jijini
Dar es Salaam na kufanya mazungumzo naye.
Katibu
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas
Kashililah (kulia) akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Rone
Plot wakati wa chakula cha mchana katika hoteli ya Kilimanjaro iliyopo
jijini Dar es Salaam.
Katibu
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas
Kashililah (kulia) akimkabidhi zawadi ya trei ya kubebea vinywaji mke wa
Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Bi. Shosh Plot wakati wa chakula
cha mchana katika hoteli ya Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam.
Katibu
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas
Kashililah (kulia) akipokea zawadi toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la
Israel, Ronen Plot wakati wa chakula cha mchana katika hoteli ya
Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam.
Katibu
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas
Kashililah (wa pili kulia)akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi
Mkuu wa Bunge la Israel, Ronen Plot (wa pili kushoto) wakati wa chakula
cha mchana katika hoteli ya Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Naibu Katibu wa Bunge John Joel
SHARE
No comments:
Post a Comment