Meneja Uhusiano wa Jamii wa
Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) Bi.Neli Msuya
akizungumza na viongozi wa Jumuiya 15 za Watumia Maji zilizojengwa chini
ya mradi wa Maji Yetu uliofadhiliwa na Serikali ya Ubelgiji kwa gharama
ya shilingi Bilioni 14.5 alipokutana nao leo jijini Dar es salaam.
Meneja Uhusiano wa Jamii wa
Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) Bi.Neli Msuya
akizungumza na viongozi wa Jumuiya 15 za Watumia Maji zilizojengwa chini
ya mradi wa Maji Yetu uliofadhiliwa na Serikali ya Ubelgiji kwa gharama
ya shilingi Bilioni 14.5 alipokutana nao leo jijini Dar es salaam.
Mshauri wa Ufundi wa DAWASA –BTC
Mhandisi Praygod Mawalla akitoa elimu kwa viongozi wa Jumuiya 15 za
Watumia Maji katika jiji la Dar es salaam namna ya kuifanya miradi
wanayoisimamia ijiendeshe na kuwa endelevu kwa manufaa ya wananchi.
Mshauri wa Ufundi wa DAWASA –BTC
Manjolo Kambili akitoa akitoa ufafanuzi kuhusu Programu ya za utoaji wa
mafunzo kwa watumiaji wa Maji katika maeneo yenye miradi hiyo wakati wa
mkutano na viongozi wa Jumuiya 15 za Watumia Maji za jiji la Dar es
salaam.
Picha ya pamoja
Bi. Mecktridis Mdaku Mtaalamu
kutoka Ofisi ya Uhusiano wa Jamii wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka
Dar es salaam (DAWASA) akiwasisitiza viongozi wa Jumuiya 15 za Watumia
Maji katika jiji la Dar es salaam kupanda miti na kuiendesha miradi
katika hali ya Usafi ili kulinda afya za watumiaji wa huduma za maji.
………………………………………………………………………………………………….
Na. Aron Msigwa –MAELEZO
Dar es salaam.
Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka
Dar es salaam (DAWASA) imewataka viongozi wa Jumuiya za watumia maji
katika jiji la Dar es salaam na baadhi ya maeneo ya Kibaha na Bagamoyo
mkoani Pwani kusimamia kikamilifu mapato na matumizi ya miradi ya maji
ili kuepuka migogoro inayosababishwa na matumizi mabaya ya fedha jambo
linalochangia baadhi ya miradi kushindwa kujiendesha na kuwa kero kwa
wananchi.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini
Dar es salaam na Meneja Uhusiano wa Jamii wa Mamlaka hiyo Bi.Neli Msuya
wakati akitoa elimu kwa viongozi hao kuhusu uendelezaji wa miradi
inayosimamiwa na Jumuiya 15 za Watumia Maji zilizojengwa chini ya mradi
wa Maji Yetu kwa ufadhili wa Serikali ya Ubelgiji.
Amesema DAWASA imekukutana
viongozi hao kuwakumbusha wajibu walio nao katika kuhakikisha miradi
wanayoisimamia inakidhi matarajio ya wananchi kwa kutoa huduma bora na
kujiendesha kwa faida kwa na kuwafikia wananchi wengi zaidi.
“Kwa kuzingatia idadi ya watu
zaidi ya Laki mbili (200,000) wanaohudumiwa na mradi huu kwa kupata
maji safi na salama na gharama kubwa iliyotumika kuanzisha mradi huu
shilingi Bilioni 14.5 ,tumeona kuna umuhimu wa kuendelea kuweka
msisitizo wa uangalizi kwa kuwa miradi hii ni muhimu na iko kwa
wananchi” Amesisitiza.
Amewaeleza viongozi hao kuwa
majukumu ya DAWASA kama mmiliki wa miundombinu ya majisafi na majitaka
ni kugharamia matengenezo makubwa na kufanya uwekezaji wa kupanua
miundombinu ya majisafi na majitaka jijini Dar es Salaam na maeneo
yaliyoainishwa chini ya Sheria ya DAWASA Namba.20 ya Mwaka 2001.
Bi. Neli amefafanua kuwa DAWASA
iliingia mkataba wa uendeshaji na Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es
salaam (DAWASCO) kutoa huduma ya uondoshaji wa majitaka katikA jiji la
Dar es salaam, Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani.
Aidha, amesema kupitia mkataba
huo, DAWASCO huuza maji kwa wateja, kutayarisha Ankara za maji,
kukusanya maduhuli, kulipia gharama za uendeshaji na kufanya matengenezo
ya mfumo mzima wa usambazaji maji na uondoshaji majitaka katika maeneo
mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.
“Kupitia elimu inayotolewa leo
mtagundua kuwa ninyi ni muhimu katika kuwahudumia wananchi, mtaona kuwa
ninyi ni DAWASCO ndogondogo kwenye maeneo yenu kwa kuwa mnauza maji kwa
wateja, mnatayarisha Ankara za maji , mnakusanya fedha za malipo ya
huduma mnafanya matengenezo ya mifumo ya maji kwa wateja wenu”
Amesisitiza.
Amesema kwa sasa DAWASA imewekeza
kwenye miradi mikubwa na kupanua chanzo cha Maji cha Ruvu chini ambacho
huzalisha lita milioni 270 kwa siku, ujenzi wa Bomba kubwa lenye urefu
wa Kilometa 56 kutoka Ruvu Chini hadi matenki yaliyopo chuo Kikuu Ardhi
jijini Dar es salaam.
Aidha amesema kwa upande wa Ruvu
juu maboresho makubwa yamefanyika kwa kupanua mitambo ya uzalishaji
ambayo sasa itazalisha lita milioni 196 kutoka milioni 82 kwa siku.
Ameongeza kuwa upande wa maeneo
ya kaskazini na kusini mwa jiji la Dar es salaam kuelekea wilaya ya
Mkuranga DAWASA inaendelea kuwekeza katika uchimbaji wa visima virefu
vya maji na kuweka mifumo ya usambazaji wa maji ili kuwawezesha wananchi
kupata maji safi na salama kwa gharama nafuu.
Kwa upande wake Mshauri wa Miradi
ya Maji kutoka DAWASA –BTC Bw. Manjolo Kambili amewaeleza viongozi hao
kuwa wao kama viongozi wa Jumuiya za watumia maji wanatakiwa kufuata
sheria na taratibu za Serikali kwa kuwa miradi hiyo ni ya Serikali.
Ameeleza kuwa jukumu la kusimamia
na miradi hiyo liko kisheria hivyo viongozi hao wanapaswa kutekeleza
kikamilifu majukumu yao likiwemo la kuhakikisha kuwa miradi yote
inaajiri wahasibu wenye taaluma kwa lengo la kuandika na kutunza
kumbukumbu za kila siku zinazohusu mapato na matumizi yao.
“Naomba nisisitize katika hili,
nyie mmepewa jukumu la kusimamia miradi ya maji ya Serikali, lazima
mlitambue hili miradi yenu itakaguliwa na wataalamu ndio maana
tuliwaomba muajiri wahasibu kwa kuwa vitabu vyenu vitakaguliwa kujua
mwenendo wa mapato na matumizi yenu” Amesisitiza.
Amewataka viongozi hao
kuhakikisha kuwa kila mradi wa jumuiya unakuwa na akaunti ya Benki
pamoja na kusimamia suala la utoaji wa risiti halali zenye nembo za
jumuiya husika ili kuweka uwazi na imani wa walipiaji Ankara za maji.
Naye Afisa Uhusiano na Jamii wa
Mamlaka hiyo Bi. Mecktridis Mdaku amewasisitiza viongozi hao kusimamia
suala la Usafi wa mazingira, upandaji wa miti na utunzaji wa vituo vya
miradi, majengo na miundombinu ya maji ili kuwakinga wananchi dhidi ya
magonjwa ya milipuko ikiwemo.
“Ninyi kama viongozi wa Kamati za
miradi ya maji lazima msimamie suala la usafi wa mazingira ili maeneo
ya miradi yavutie pia kuwakinga wateja wenu na ugonjwa wa kipindupindu”
Amesisitiza Bi. Mdaku.
Ametoa wito kwa viongozi hao
kuepuka kuyatumia majengo ya miradi ya maji ya wananchi kwa shughuli
nyingine nje ya maji ikiwemo kuhifadhi na kufanyia biashara ya mkaa.
SHARE
No comments:
Post a Comment