Mkurugenzi
wa Mauzo wa Kampuni ya Jumbo Camera House, Mathias Luoga akionesha
vifaa mbalimbali vya kamera wakati wa uzinduzi wa duka jipya lililopo
Jengo la NSSF Benjamin Mkapa, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi
wa kampuni hiyo, Sara Filikunjombe, mke wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la
Ludewa, marehemu Deo Filikunjombe ambaye pia mmiliki wa kampuni hiyo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA: KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mke wa
marehemu Filikunjombe, Sara (wa pili kulia) akiwa na Mkurugenzi wa
Kampuni ya Benchmark Prodaction, Ritta Poulsen (wa pili kushoto), Kaimu
Mkurugenzi wa Kampuni ya Jumbo Camera House, Paul Buckendahl (kushoto)
pamoja na Mkurugenzi wa Mauzo wa Kampuni hiyo, Mathias Luoga
wakigongeana glasi zenye Champagn wakati wa hafla hiyo.
Wageni
waalikwa wakioneshwa moja ya kamera na vifaa vyake inayouzwa katika duka
hilo kubwa la aina yake kwa Afrika Mashariki, Kati na Kusini.
Paul akiwaongoza wageni waalikwa kusimama kwa dakika moja kumkumbuka marehemu Deo Filikunjombe.
Mgeni rasimi katika hafla hiyo, Ritta Poulsen akihutubia wakati wa uzinduzi wa duka hilo.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment