Kocha wa
kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ ambaye
ni mratibu wa mpambano wa mabondia Mada Maugo kushoto na Abdallah Pazi
akiwainuwa mikono juu kwa ajili ya kutambulisha mpambano wao wa ubingwa
wa U.B.O Afrika utakaopigwa siku ya sikukuu ya pasaka katika uwanja wa
ndani wa Taifa march 27
Kocha wa
kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ ambaye
ni mratibu wa mpambano wa mabondia Mada Maugo kushoto na Abdallah Pazi
akiwainuwa mikono juu kwa ajili ya kutambulisha mpambano wao wa ubingwa
wa U.B.O Afrika utakaopigwa siku ya sikukuu ya pasaka katika uwanja wa
ndani wa Taifa march 27. Picha na SUPER D BOXING NEWS
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA
Mada Maugo na Abdallah Pazi ‘Mfalme wa waalamu’ wamendelea kutambiana
kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika siku ya March 27 sikukuu ya
Pasaka katika uwanja wa ndani wa Taifa akizungumza wakati wa kutambulisha mpambano wao uho
Bondia
Mada Maugo amesema kuwa Pazi i mtoto mdogo sana katika ulimwengu wa
masumbwi nchini hivyo inambidi afanye mazoezi ya kutosha ili avuke japo
raundi ya nne mana sitakuwa na msalia mtume wakati wa kupambana pia
naomba mashabiki zangu wafike mapema kwa ajili yakuona
ninavyomsambalatisha Pazi mapema mana nimewapa bonanzi ya raundi nne
mashabiki zangu akijibu mapigo
hayo bondia Pazi amesema yeye kwa sasa ndio anatamba nchini hivyo yeye
ni mfalme na akuna wa kuusambalatisha ufalme wake kwani kilicho mkuta
bondia aliempiga China kwa K.o ya raundi ya tatu ndicho kitakacho mkuta
yeye kwani kesha zeeka sasa ni wakati wa damu changa pekee nae
mratibu wa mpambano uho Rajabu Mhamila ‘Super D’ amesema mbali y
mpambano uho unaosubiliwa kwa hamu na mashabiki lukuku kutakuwa na
mipambano ya kukata na shoka ambapo
bondia Nassibu Ramadhani atakumbana na Fansic Miyeyusho na bingwa wa
mikanda miwili ya Afrika U.B.O na WPBF, Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’
atkumbana na Deo Samweli na Pius Kazaula atakumbana na Seba Temba mpambano mwingine utawakutanisha Cosmas Cheka na Mohamed Matumla
Katika
mpambano uho kutakuwa na uhuzwaji wa vifaa vya mchezo wa ngumi pamoja na
DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kwa ajili ya kutambua sheria
mbalimbali za mchezo zitakazokuwa zikitolewa bule kwa mabondia
watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa galama nafuu. (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment