Shirika
la ndege la gharama nafuu Afrika, Fastjet Tanzania limeongeza idadi ya
safari zake kwenye njia yake ya Dar es Salaam na Nairobi ikiwa ni
mwitikIo mkubwa kwa mahitaji ya abiria.
Kuanzia
Machi 21 fastjet itakuwa inafanya safari zake mara mbili kwa siku kwenda
na kurudi kati ya miji hiyo miwili kila siku ndani ya wiki na hivyo
kufanya safari zake kuwa ni 28 kwa wiki kati ya Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na Uwanja wa Kimataifa
wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.
Shirika
hilo ambalo hadi sasa linafanya safari moja kila siku kati ya miji hiyo
miwili, limeongeza masafa yake ya kuruka ili kuwapatia abiria huduma
nzuri nyakati za asubuhi na jioni.
Kwenye
safari ya asubuhi, ndege itakuwa inaondoka Dar es Salaam saa 12.00 na
kutua Nairobi saa 1.20. Aidha, safari ya kurudi itaanza saa 1.50 na
itatua Dar es Salaam saa 3.15.
Aidha,
safari mpya za jioni ndege itakuwa inaondoka Dar es Salaam saa 2.15 na
kutua Nairobi saa 3.35. Safari ya kuridi ndege itaondoka Nairobi saa
4.05 na itatua Dar es Salaam saa 5.30.
Kupanuka
kwa ratiba hiyo kutawezesha kusafirisha takribani abiria 19,000 kila
mwezi kupitia safari za fastjet kati ya hiyo miji miwili, na hivyo
kuwapa wasafiri njia nzuri zaidi na mbadala wa safari kwa nauli
wanayoimudu.
“Kila
mara tumekuwa tunaahidi kuongeza masafa yetu ya njia yetu kati ya Dar es
salaam na Nairobi kutokana na mahitaji ya wateja kuongezeka
kunakosababisha na nauli wanayoimudu, usalama, kasi na huduma kwa
wakati,” alisema Meneja Mkuu wa Fastjet Tanzania, John Corse.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment