WAZEE
na walemavu wa viungo wanaoishi katika mazingira magumu katika kambi ya
Bukumbi iliyopo Wilaya ya Misungwi mkoani hapa, wamekumbukwa kwa
kusaidiwa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Sh. Milioni 54.
Hafla
ya kukabidhi vifaa hivyo ilifanyika jana mbele ya mke wa Rais Dk. John
Magufuli, Janet Magufuli katika kambi hiyo yenye watu wenye mahitaji
mbalimbali ya kijamii.
Akizungumza
wakati akikabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles
Kimei, alivitaja vifaa vilivyotolewa kuwa ni Mchele tani 6, Unga wa
mahindi 6, Maharagwe tani 3, Sukari tani 2 na nusu na mafuta ya kula
lita 1000.
Dk.
Kimei alitaja vifaa vingine vilivyotolewa katika kambi hiyo ya wazee
kuwa ni pamoja na umeme wa jua na kudai kwamba hatawataishia hapo
wataendelea kutoa misaada ikiwemo kukarabati majengo ya makazi hayo.
Kwa
upande wake, Janet Magufuli, alisema kuwa katika kipindi kichache
alichozunguka katika kambi 17 nchini alikuta kambi hizo zinakabiliwa na
changamoto nyingine ikiwemo ya maladhi.
Alisema
kuwa hali hiyo ilisababisha kuanza kutafuta wadau mbalimbali ikiwemo
benki hiyo ambayo ilichukua jukumu hilo la kuwasaidia watu hao,
wanaokabiliwa na changamoto nyingi.
Kambi
hiyo iliyoanzishwa mwaka 1974 kwa sasa ina zaidi ya Wazee 100, kwa muda
mrefu sasa watu hao wamekuwa ni omba omba katika maeneo mbalimbali ya
Jiji la Mwanza.
Vitu
hivi endapo kama havita chuchukuliwa hatua na kuwasaidia yanaweza
kuwasababishia magonjwa mbalimbali, sasa nilazima wadau wengine
wajitokeze kusaidia kambi hizi, alisema mama Magufuli.
Mke wa
Rais Dk. John Magufuli, Janet Magufuli na Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa
Mwanza, wakati alipowasili katika kambi ya Wazee ya Bukumbi iliyopo
Wilaya ya Misungwi, Jijini Mwanza.
Sehemu ya Misaada iliyotolewa na Benki ya CRDB kwa kambi ya Wazee ya Bukumbi iliyopo Wilaya ya Misungwi, Jijini Mwanza.
Mke wa
Rais Dk. John Magufuli, Janet Magufuli (wa pili kulia) akikabidhiwa
pannel ya Solar kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt.
Charles Kimei, ikiwa ni maalum kwa kusaidia kambi ya Wazee ya Bukumbi
iliyopo Wilaya ya Misungwi, Jijini Mwanza. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mkoa
wa Mwanza, Magese Mulongo (wa pili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya
Misungwi, Mwajuma Nyiruka.
Mke wa
Rais Dk. John Magufuli, Janet Magufuli, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu
wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei, walipokutana kwenye kambi ya
Wazee ya Bukumbi iliyopo Wilaya ya Misungwi, Jijini Mwanza.
Mkurugenzi
Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei, akiwasalimia baadhi ya Wazee
wanaolelewa kwenye kambi ya Wazee ya Bukumbi iliyopo Wilaya ya
Misungwi, Jijini Mwanza.
Mke wa
Rais Dk. John Magufuli, Janet Magufuli, akiwahutubia wananchi wakati wa
hafla ya kukabidhi misaada kwenye kambi ya Wazee ya Bukumbi iliyopo
Wilaya ya Misungwi, Jijini Mwanza.
Mke wa
Rais Dk. John Magufuli, Janet Magufuli (wa pili kulia) akikabidhiwa
sehemu ya misaada mbalimbali kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya
CRDB, Dkt. Charles Kimei, kwa ajili ya kusaidia kambi ya Wazee ya
Bukumbi iliyopo Wilaya ya Misungwi, Jijini Mwanza. Kulia ni Mkuu wa Mkoa
wa Mwanza, Magesa Mulongo.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei, akizungumza.
SHARE
No comments:
Post a Comment