Mkurugenzi
wa kampuni ya utalii ya Viola,Violet .c. Mfuko akizima mshumaa
alipokuwa akiazimisha siku yake ya kuzaliwa iliyofanyikia katika
hospitali ya mt.Meru jijini Arusha jana
Mkurugenzi
wa kampuni ya utalii ya Viola,Violet .C. Mfuko akikata keki alipokuwa
akisherekea siku yake ya kuzaliwa iliyo fanyika katika hospitali ya
mt.Meru iliyoko jijini Arusha jana.
Mkurugenzi
wa kampuni ya utalii ya Viola,Violet Mfuko akimlisha keki mkurugenzi
mwenzake, ambae ni (mme wake) ndugu Kim Godwin Fute,alipokuwa
akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa iliyo fanyika katika hospitali ya
mt.Meru iliyoko jijini Arusha jana.
Mkurugenzi
wa kampuni ya utalii ya Viola,Violet Mfuko akimkabidhi shuka mganga
mkuu mfawidhi wa hospital ya mt.Meru dr.Jackline Urio alipokuwa
akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa jana.
Picha ya pamoja ya marafiki wa Violet ilipigwa.
Mkurugenzi
wa kampuni ya utalii ya Viola,Violet Mfuko akimuombea mgonjwa Frida
Shayo alipotembelea hospitali ya mt.Meru alipokuwa akiadhimisha siku
yake ya kuzaliwa jana.
Mkurugenzi
Viola Mfuko anamlisha keki Habibya Fadhili alipotembelea hospital ya
mt.Meru alipokuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa jana.
********************
Katika
kuelekea maadhimisho ya kilele cha siku ya wanawake duniani machi nane
baadhi ya wanawake jijini Arusha wanaadhimisha siku hiyo kwa matukio
mbalimbali ambapo mwanamke mjasiriamali wa jijini humo Violet Mfuko
amejitolea kujenga sehemu ya kusubiria na kufanyia ibada katika mochwari
ya hospitali ya mkoa wa Arusha ya mountmeru pamoja na mashimo nane ya
vyoo katika sehemu hiyo.
Akiwa
ameongozana na wakina mama wengine walianzia kutoa msaada wa vitu
mbalimbali katika wodi ya wanawake na watoto ambapo Viola anasema baada
ya kutembelea sehemu ya mochwari katika hospitali hiyo aligundua
changamoto hiyo ambayo ilimgusa na kuamua kujitolea kuanza ujenzi wa
jengo hilo kuanzia jumatatu machi 7 ambalo litagharimu kiasi cha
shilingi milioni 50.
Alisema
ameamua kujikita katika kusaidia jamii badala ya kutumia fedha zake
katika mambo ambayo hayana faida kwa jamii na kysisitiza kuwa baada ya
kupewa ramani na uongozi wa hospitali ataanza ujenzi jumatatu machi 7
mwaka huu.
Alisema
baada ya kujionea adha wsnayoipata wafiwa kukosa sehemu ya kusubiria
miili ya marehemu na vyoo vinavyotumika kuwa ndani ya mochwari aliguswa
na suala hilo na kuamua kujenga vyo na sehemu hiyo.
"Tayari
nimeshapokea ramani nitaanza ujenzi jumatatu nawaomba wana Arusha mnipe
ushirikiano tuweze kumsaidia rais magufuli yeye alianza na muhimbili
sisi tumeamua kumsaidia hospitali yetu ya mkoa"alisema Violet.
Viola
ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Viola car hire yenye makao makuu
yake jijini Arusha anatumia siku yake ya kuzaliwa kutoa msaada katika
hospitali hiyo na kutoa wito kwa wakazi wa mji wa Arusha kuanza kuisadia
serikali kuboresha sekta ya afya kwa kuwa sekta hiyo inachangamoto
nyingi.
"Mimi
nikiwa ni mwanamke ninajua changamoto nyingi zinazotukaabili kina mama
na watoto ambapo naamini ukimsaidia mama na mtoto umegusa jamii
nzima"alisema Violet
Hata
hivyo baadhi ya wajasiriamali wengine wa jijini humo wanaunga mkono
jitihada za mwanamama huyo ambapo daktari Edmund Matafu anajitolea
mashine mbili za hewa safi kwa ajili ya kusaidia watoto wanaozaliwa
kabla ya muda yaani njiti.
Mganga
mfawidhi wa hospitali ya mkoa ya mountmeru Jackline Uriyo amemshukuru
Violet na Dakta Matafu kwa msaada wao ambao amesema umefika wakati
mwafaka.
"Kwa
niaba ya uongozi wa hospitali ya mountmeru tunatoa shukrani za dhati
kwa Viola na dakta Matafu tunawaomba waendelee na moyo huo lakini
tunatoa wito kwa watu wengine wenye mapenzi mema kuisaidia hospitali ya
mkoa kwani inalabiliw na changamoto nyingi"alisema Uriyo
Mbali
na msaada huo Viola pia ametoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo
mashuka mia mbili,sabuni,mchele,juisi soda mablanketi vyote vikiwa na
thamani ya shilingi milioni kumi.
SHARE
No comments:
Post a Comment