Wanajeshi wa Kenya wakiwa kwenye moja ya kambi yao kukabiliana na wapiganaji wa Al-Shabab
Na RFI
Mwandishi
wa habari wa Somalia, Hassan Hanafi Haji, aliejiunga na wapiganaji wa
kundi la Kiislam la Al Shabab, amehukumiwa adhabu ya kifo Alhamisi hii
Machi 3 mjini Mogadishu kwa kosa la kupanga mauaji ya wafanyakazi
wenzake 5 kati ya mwaka 2007 na 2010.
"Hassan
Hanafi amehukumiwa adhabu ya kifo baada ya mahakama kumkuta na hatia ya
mashtaka yote dhidi yake," amesema jaji Hassan Ali. "Vielelezo vya
ushahidi na mashahidi vinaonyesha kuwa alihusika katika kwa kiwango
kikubwa katika mpango na utekelezaji wa mauaji ya waandishi wa habari,
ameongeza Hassan Ali". Somalia ni nchi hatari zaidi duniani kwa
waandishi wa habari.
Kwa
mujibu wa mahakama, Hassan Hanafi Haji alitambua makosa yake pamoja na
kuwa katika kundi la Al Shabab. Bado anaweza kukata rufaa. Nchini
Somalia, kawaida, watu wanaohukumiwa adhabu ya kifo, hupigwa risasi.
Hassan
Hanafi Haji alikamatwa Agosti 2014 katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, na
alisafirishwa nchini Somalia mwishoni mwa mwaka huo. Alhamisi hii,
waandishi wa habari kadhaa wamehudhuria kesi hiyo mjini Mogadishu.
Somalia
ni moja ya nchi hatari zaidi kwa waandishi wa habari: waandishi wa
habari 33 kutoka Somalia wameuawa nchini humo tangu mwaka 2007 ya kundi
la Al Shabab kuzidisha mashambulizi yake katika maeneo mablimbali nchi
Somalia, kwa mujibu wa Shirika la Kulinda Waandishi wa Habari (CPJ).
Kundi la
Al Shabab, lenye uhusiano na al-Qaida, wameapa kuivunja serikali dhaifu
ya Somalia, inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa na kusaidiwa na
kikosi imara cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika (AMISOM) chenye wanajeshi
22,000.
Wapiganaji
wa Al Shabab, hivi karibuni, waliendesha mashambulizi makubwa dhidi ya
kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika (AMISOM) na kutekeleza
mashambulizi yaliosababisha vifo vingi vya watu dhidi hoteli na migahawa
mjini Mogadishu. Wamekua wakirusha ujumbe wao na itikadi zao kupitia
radio yao na video za propaganda ambazo wamekua wakirusha kwenye mtandao
wao.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment