Mbunge
wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo akifungua mlango wa gari la wagonjwa kabla ya kulikabidhi rasmi.
Daktari
Bingwa wa huduma za dharura na Majanga, Dkt. Christopher Mnzava (kulia)
akizungumza jambo wakati wa hafla ya kukabidhi gari la wagonjwa la
Kituo cha Afya cha Murangi. Kushoto ni Mbunge wa Musoma Vijijini na
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
Mbunge
wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo akimkabidhi nyaraka za gari la wagonjwa la Kituo cha Afya cha
Murangi, Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho, Dkt. Naomi Nyanchara.
Gari
la wagonjwa la Kituo cha Afya cha Murangi ambalo limekabidhiwa hivi
karibuni. Gari la namna hiyo na la pili nchini na huku lingine lipo
Hospitali ya Muhimbili.
Vifaa vya kisasa kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa katika gari la wagonjwa la Kituo cha Afya cha Murangi.
Mbunge
wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo akilikagua gari la wagonjwa kabla ya kulikabidhi.
Mbunge
wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo amekabidhi gari la kisasa la wagonjwa kwa Kituo cha Afya cha
Murangi, Wilaya ya Musoma Vijijini .
Makabidhiano
hayo yamefanyika hivi karibuni kituoni hapo na kushuhudiwa na wananchi
mbalimbali kutoka maeneo tofauti ya wilaya hiyo baada ya gari hiyo
kukaguliwa kwa kina na Daktari Bingwa wa huduma za dharura na Majanga,
Dkt. Christopher Mnzava na kujiridhisha kwamba lipo tayari kwa kuanza
kutumika kutoa huduma husika.
Akizungumza
kabla ya makabidhiano hayo, Profesa Muhongo alisema gari hilo
limetolewa na Serikali ya Japan kwa ajili ya wananchi wa jimbo la Musoma
Vijijini lengo likiwa ni kusaidia wananchi hao kuondokana na usumbufu
waliokuwa wakiupata.
Alisema
kwamba Serikali hiyo ya Japan kupitilia Balozi wake nchini Tanzania,
imeahidi kwamba endapo gari hilo litatunzwa na kutumika kwa lengo
lililokusudiwa ndani ya kipindi cha miezi sita, wananchi hao wataongezwa
gari linguine la aina hiyo.
Profesa
Muhongo aliwaagiza wananchi wa jimboni humo kuwa walinzi wa gari hilo
ili kuhakikisha linatunzwa vizuri na vilevile linatumika kwa malengo
yaliyokusudiwa.
“Ninamuomba
Dkt. Mnzava awe anakuja huku mara kwa mara kwa ajili ya kuligakua. Nyie
tutakaowakabidhi endapo mtatatizwa na jambo kwenye gari hilo
muwasiliane nae ili awapatie maelekezo ya nini cha kufanya.”
Akizungumza
wakati wa makabidhiano hayo, Dkt. Mnzava alimpongeza Mbunge huyo kwa
juhudi zake za kuhakikisha anamaliza kero mbalimbali zilizokuwa
zikiwakabili wananchi wa jimboni humo hususan katika suala la afya.
Alisema
kuwa amelikagua gari hilo na kwamba ni gari la kisasa na ni tofauti na
magari mengine ya wagonjwa ambayo yapo katika hospitali mbalimbali
nchini.
Aliongeza
kuwa vifaa vilivyomo ndani ya gari hilo ni adimu na hivyo inapasa
watakaokabidhiwa walitunze. “Kwa hapa Tanzania gari la aina hii lipo
hospitali ya Muhimbili peke yake; hivyo kwa sasa yapo mawili moja ni
hili la Murangi na lingine ni la Muhimbili,” alisema.
Alisema
wananchi wa Musoma Vijijini wanayo bahati kubwa kuwa na Mbunge ambaye
anajitahidi kushughulikia kero zao kwa kuwatafutia ufumbuzi wa kudumu.
Aidha,
kwa upande wa wananchi waliojitokeza kushuhudia makabidhiano hayo,
walimpongeza Profesa Muhongo kwa juhudi zake alizozionyesha tangu
amechaguliwa za kuwaletea maendeleo.
Nyanjiga
Mgeta ambaye alikuwa Kituoni hapo kwa ajili ya kupatiwa matibabu
alizungumza na mwandishi wa habari hii na kueleza kuridhishwa kwake na
kasi ya maendeleo ya mbunge huyo.
Mgeta
alisema hapo awali iliwalazimu wakodi magari ili kufikisha wagonjwa
mahututi hospitalini jambo ambalo ni gharama kubwa na vile vile
upatikanaji wa magari jimboni humo ni mgumu.
Mwananchi
mwingine aliyefahamika kwa jina la Eliza Chilyamkobi alimpongeza
Profesa Muhongo na kueleza kwamba gari hilo ni mkombozi kwao na vilevile
alimuahidi ushirikiano zaidi na ulinzi wa gari hilo.
Aidha,
Profesa Muhongo alisema ifikapo tarehe 6 mwezi huu timu ya madaktari
bingwa wapatao sita kutoka China itawasili kituoni hapo kwa ajili ya
kutoa huduma ya uchunguzi wa afya na kutoa tiba kwa maradhi mbalimbali.
Alisema
madaktari hao vilevile wanakuja na madawa ambayo watayakabidhi kwa
wahusika kituoni hapo na huku akiwataka wananchi hao kujitokeza kwa
wingi ili kupatiwa tiba bila gharama yoyote.
Katika
hafla hiyo, Profesa Muhongo alichangia bati 50 na mifuko ya saruji 234
kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Wadi ya kina mama na watoto.
SHARE
No comments:
Post a Comment