Na.catherine Sungura,Kyela
Wananchi
wa wilaya ya kyela wametakiwa kuachana na mila potofu na kupelekea
kufanya mauaji ya watu kwa kuhusisha ugonjwa wa kipindupindu ni ugonjwa
unaoletwa kwa imani ya kishirikina
Hayo
yamesemwa leo na waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na
watoto Ummy Mwalimu,wakati alipofanya ziara katika wilaya hii na kuongea
na watendaji wa halmashauri.
Mh.Ummy
alisema ameshangazwa na baadhi ya wananchi katika kijiji cha unyakyusa
kujichukulia sheria mkononi na kuwauwa wanawake watatu kwa madai ndio
wanaoneza ugonjwa huo.
Naye mkuu
wa wilaya ya kyela dkt. Thea Ntara alisema kamati yake ya ulinzi na
usalama imeshawakamata watuhumiwa wawili wa tukio hilo na kuwafikisha
mahakamani ingawa bado mtuhumiwa mmoja aliyekimbilia nchi jirani ya
malawi anatafutwa.
Matukio hayo yametokea mwezi februari na machi mwaka huu.
Wilaya ya kyela ilipokea mgonjwa wa kipindupindu novemba 2015 na hadi kufikia machi 2016 jumla ya wagonjwa 405 waliugua ambapo vifo vilikua 8. Kwa sasa wilaya hii haina mgonjwa wa kipindupindu
Wilaya ya kyela ilipokea mgonjwa wa kipindupindu novemba 2015 na hadi kufikia machi 2016 jumla ya wagonjwa 405 waliugua ambapo vifo vilikua 8. Kwa sasa wilaya hii haina mgonjwa wa kipindupindu
Hali ya
kipindupindu nchini imekua ni tatizo kubwa nchini,takribani mikoa yote
tanzania bara imekubwa na ugonjwa huu tangu ulipotiwe mwezi agosti mwaka
jana,isipokuwa kwa mkoa wa Ruvuma na Njombe ambapo hawajaripoti mgonjwa
wowote hadi Sasa
Ripoti ya
wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto ya tarehe 4
machi mwaka huu inaonesha jumla ya wagonjwa 20,294 wametolewa taarifa na
kati ya hao 320 wamepoteza maisha.
Kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka,mwenendo wa kipindupindu unaashiria idadi ya wagonjwa nchini inaongezeka.(P.T)
Kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka,mwenendo wa kipindupindu unaashiria idadi ya wagonjwa nchini inaongezeka.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment