
Mkuu wa
Mkoa wa Geita Meja Generali Mstaafu Ezekiel Kyungu akishuhudia mabati
yaliyotolewa ma Mfuko wa Pensheni LAPF kwa ajili ya ujenzi wa madarasa
wilayani Geita ikiwa jitihada za Mfuko wa LAPF kuunga mkono jitihada za
Serikali kutoa elimu bure. Jumla ya mabati 300 yenye thamani ya Shs.
7,000,000/= yalikabidhiwa.

Mkuu wa
Mkoa wa Geita Meja Generali Mstaafu Ezekiel Kyungu akikagua mabati
yaliyokabidhiwa kama msaada na mfuko wa Pensheni wa LAPF wilayani Geita,
kulia ni Meneja Masoko wa Mfuko wa LAPF Bw. James Mlowe wengine ni
maofisa kutoka wilaya ya Geita.

Mkuu wa
Mkoa wa Geita Meja Generali Mstaafu Ezekiel Kyungu akiteta jambo na
Meneja Masoko wa Mfuko wa Pensheni LAPF pamoja na mbalimbali wa Wilaya
ya Geita mara baada ya makabidhiano ya msaada wa mabati kwa ajili ya
ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Mkuu wa
Mkoa wa Geita akitoa neno la shikrani kwa Mfuko wa Pensheni LAPF kwa
msaada wa mabati 300 yanayotosheleza kuezeka vyumba sita (6) vya
madarasa yanayoweza kuchukua wanafunzi 45 kwa kila chumba na hivyo
kupunguza tatizo la ukosefu wa mazingira bora ya kufundishia. PICHA NA MPIGA PICHA WETU (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment