
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akisalimiana na wafanyakazi wa Mashirika mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa yanayoshirikiana na Serikali ya Tanzania kutoa huduma katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, iliyoko wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.Naibu Waziri yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ikiwemo kutembelea kambi za wakimbizi zilizopo ndani ya mkoa wa Kigoma.

Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia),
akizungumza na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ibungho, Anatory
Nsamizanala(wa kwanza kushoto), mara baada ya kufika katika shule hiyo
inayotoa elimu ya awali katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu, iliyopo
wilayani Kasulu, mkoani Kigoma. Naibu Waziri yuko mkoani Kigoma kwa
ziara ya kikazi ikiwemo kutembelea kambi za wakimbizi zilizopo ndani ya
mkoa wa Kigoma.Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Gerald
Guninita.

Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(kulia),
akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Ruth Msafiri (wa pili kulia),
kukagua ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Mabamba kilichopo wilayani
Kibondo,mkoani Kigoma.Kituo hicho cha Polisi kinajengwa kwa ushirikiano
kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Kimataifa la kuhudumia
Wakimbizi(UNHCR). Naibu Waziri yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi
ikiwemo kutembelea kambi za wakimbizi zilizopo ndani ya mkoa wa Kigoma.

Mkimbizi
kutoka nchini Burundi, Exavery Christopher (aliyevaa kofia nyeupe),
akitoa maelezo mbele ya Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(wa kwanza kushoto), wakati akijibu maswali
aliyoulizwa na Naibu Waziri muda mfupi baada ya kuwasili katika kituo
cha Uhamiaji cha Mabamba tayari kwa kusajiliwa kabla ya kupelekwa
kambini.Wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kibondo, Ruth
Msafiri. Naibu Waziri yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ikiwemo
kutembelea kambi za wakimbizi zilizopo ndani ya mkoa wa Kigoma.Ziara
iliofanyika tarehe 30/3/2016.
(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi) (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment