
Mkuu wa
wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amemsweka rumande Muhandisi wa
halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Simoni Ngagani, baada ya kupuuza
agizo lake la kufanya maandalizi mapema ya kununua kokoto na Saruji kwa
ajili ya kusimika mapipa 50 ya kutunzia uchafu kwenye mitaa mbalimbali
katika manispaa ya Shinyanga ikiwemo eneo kituo cha mabasi yaendayo
wilayani.
Matiro alimuagiza Mhandisi huyo
kufanya maandalizi hayo mapema mbele ya mkurugenzi wake wa manispaa ya
Shinyanga Kalinjuna Lewis, kuwa ataandaa vifaa hivyo majira ya saa moja
asubuhi ili zoezi kukusimika mapipa hayo likamilike haraka, na baada ya
hapo wafanye usafi wa mazingira lakini agizo lake mhandisi huyo
akapuuza.Mkuu huyo alipomhoji mhandisi huyo kwanini alipuuzia agizo lake la kufanya maandalizi mapema, mhandisi huyo alianza kujikanyaga kanyaga akidai sababu iliyomkwamisha ni kukosekana kwa pesa za kununua kokoto na saruji kwani mvua kubwa ilinyesha na kushindwa kwenda benki, na alivyoamka asubuhi ndipo atakafuta dhana hizo.
Hata hivyo mkuu huyo hakuridhika na majibu hayo ndipo DC alipochukua uamuzi ya kumsweka rumande kwa kumuagiza mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya Shinyanga kumkamata na kumuweka ndani mhandisi huyo wa ujenzi manispaa hiyo Samson Ngagani kwa kosa la kuchelewesha maandalizi ya vifaa vya ujenzi vilivyopangwa kutumika kusimika mapipa ya taka.
“Hawezekani tukubaliane tuamke mapema ili tufanye kazi hii haraka na pia tuingie Mitaani kufanya usafi, ambapo mimi nimeamka saa 11 nikajiandaa harafu wewe una kuja saa mbili tena bila ya kufanya maandalizi yeyote hii si kunidharau hivyo naagiza OCD mkamate akakae Rumande kwanza ili liwe fundisho kwa wengine” ,alisema Matiro.
Katika uzinduzi huo Matiro alisema mapipa hayo ya taka ambayo idadi yake ni zaidi ya 50 yatawekwa katika maeneo mbali mbali ya manispaa ya Shinyanga na wananchi wanatakiwa kuyalinda.
Awali akiongea katika uzinduzi huo, mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna alisema mapipa hayo yamepatikana kutokana na wadau mbali mbali kujitolea kuchangia baada ya kuhamasishwa na mkuu huyo wa wilaya ambapo pipa moja limegharimu shilingi elfu 90.
Naye afisa afya wa manispaa ya shinyanga Elly Nakuzelwa alisema lengo la kuweka mapipa hayo ya taka ni kuhakikisha manispaa ya Shinyanga inakuwa katika hali ya usafi ili kuondoa magonjwa ya miripuko yanayosababishwa na uchafu ikiwemo kipindupindu.
Habari na Marco Maduhu na Veronica Natalis-Malunde1 bloG (P.T)
SHARE








No comments:
Post a Comment