TRA

TRA

Tuesday, April 12, 2016

Obama ajutia makosa ya Marekani nchini Libya

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

Obama
Rais Obama amekiri kwamba Marekani ilikosea katika kutatua mzozo Libya
Rais wa Marekani Barack Obama amekiri kwa mara ya kwanza kwamba serikali yake ilifeli katika kutatua mzozo wa Libya.
Amesema hilo huenda ndilo “kosa kubwa” zaidi alilolitenda wakati wa utawala wake.
Bw Obama amesema Marekani haikua na mpango mahususi wa jinsi taifa hilo litakavyotawaliwa baada ya kuondolewa madarakani kwa Kanali Muammar Gaddafi.
Alisema haya katika mahojiano na runinga ya Fox News kuangazia mafanikio na mapungufu ya utawala wake.
Gaddafi
Eneo la Sirte, alikozaliwa Gaddafi, lilishambuliwa sana na majeshi ya muungano
Hata hivyo ametetea hatua ya kuingilia kijeshi nchini Libya. Marekani na Muungano wa NATO zilitekeleza mashambulio ya anga kuwalinda raia baada ya kuzuka maasi dhidi ya Muammar Gaddafi mwaka 2011.
Bastola ya dhahabu ya Gaddafi ilienda wapi?Obama acheza densi ya tango Argentina
Lakini baada ya mauaji ya kiongozi huyo, Libya ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya makundi ya waasi huku makundi mawili yakiunda serikali na mabunge tofauti.
Gaddafi
Muammar Gaddafi aliuawa na wapiganaji
Katika hatua za kurejesha utulivu serikali ya muungano wa kitaifa inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa imewasili katika mji mkuu Tripoli ili kuanza mipango ya kuongoza nchi ya kurejesha hali ya kawaida.
Uchaguzi mkuu nchini Marekani utafanyika Novemba na Rais Obama atakabidhi madaraka kwa mrithi wake Januari mwakani baada ya kuongoza kwa mihula miwili.BBC

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger