Mbunge wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere (katikati) akizungumza
na waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya Habari Maelezo, jijini
Dar es Salaam. (Picha na Rabi Hume waModewjiblog)
Wananchi
wa Tanzania wametakiwa kuchangamkia nafasi za kufanya baishara zilizopo
kwa nchi za Afrika Mashariki kutokana na kuwepo makubaliano ambayo
yanawapa wananchi wa nchi za Afrika Mashariki kufanya biashara kwa
uhuru.
Hayo
yamesema na Mbuge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere na
kusema kuwa nchi za Afrika Mashariki zinashirikiana kwa mambo mbalimbali
ikiwepo umoja wa forodha, soko la pamoja, umoja wa fedha na shirikisho
wa kisiasa.
Amesema
kupitia makubaliano hayo Watanzania wana nafasi ya kwenda kufanya
baishara katika nchi zingine bila kuzuiliwa na hivyo kuwa na nafasi ya
kusambaza bishaa zao katika nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki.
“Huu ni
muda wa Watanzania kuchangamkia nafasi zilizopo za kufanya baishara kwa
nchi za Afrika Mashariki, vikwazo zilivyopo kwa sasa ni wananchi wengi
wa Afrika Mashariki bado hawana uelewa wa kutosha kuhusu hilo lakini
tumejipanga katika hilo,” amesema Nyerere.
Amesema
kwa kutambua changamoto hiyo ya wananchi wengi kutokufahamu nafasi hiyo,
wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Tanzania wataendesha programu
ya kuwaelimisha Watanzania jinsi wanavyoweza kunufaika na ushirikiano
huo.
Amesema
programu hiyo ilianza Aprili 4 na itafanyika hadi Aprili, 23 ambapo kwa
kuanza wamepanga kukutana na Kamati za Bunge, Taasisi za Elimu ya Juu,
vyombo vya habari, kutembelea soko la Kariakoo na soko la Samaki la
Feri.
Pia
Nyerere amewataka Watanzania kuwa na mazoea ya kutafuta taarifa
mbalimbali kupitia mitandao kwani kwa kufanya hivyo wanaweza kukutana na
fursa nyingi ambazo hawakuwa wakizifahamu awali.
Mbunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Shyrose Bhanji akizungumza jambo.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wakichukua habari. (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment