Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akisalimiana na Viongozi mbalimbali kwenye Ofisi za Mkuu wa Mkoa leo
Waziri
wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye leo tarehe
14 April, 2016 akiwa mkoani Kagera ahaidi kuihamishia Wizara yake
kwenye mikoa na Halmashauri za Wilaya kwa wadau wanaohusika ili
kurasmisha shughuli na majukumu ya wizara hiyo ili iweze kupata
ufanisi.
Akiongea na wadau mbalimbali wanaohusika na Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo alisema kuwa lengo la ziara yake ni kuja mikoani
kujionea changamoto mbalimbali za wizara yake ili aweze kuzifanyia kazi
kwa kuishusha wizara kwa wadau wanaohusika ili kutekeleza majukumu
yake.
Katika kikao hicho Waziri Nape alisema kuwa sekta nne ambazo ni Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo zimekuwa hazifanyi kazi zake vizuri kutokana
na watendaji wake kutokuwa na idara au vitengo vinavyohusika moja kwa
moja na kazi zao jambao ambalo linawafanya kujishikiza katika sehemu au
idara nyingine.
Waziri Nape akisaini kitabu kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Picha na Faustine Ruta, Bukoba
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Jackson Msome(kushoto) ambaye alikaimu nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera leo akitoa neno.
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akisikilizwa kwa
makini na Wadau wa Maendeleo hapa Bukoba, Picha na Faustine Ruta, Bukoba
Ndugu Willy Bukobatours Rutta,Diwani kata ya Ishozi nae alikuwepo
Kulia ni Bw. Gonzaga Meneja wa Jambo Bukoba Mkoani Kagera
Wakifuatilia jambo kwa karibu
Kaimu wa RAS Bw. Adam Swai akitoa neno
Taswira kamili
Sekta ya Habari
Mhe, Nape aliagiza Halmashauri za Wilaya kuajiri Maafisa Habari katika
Halmashauri ambazo hazina Maafisa hao, pili kuwaruhusu Maafisa hao
kuingia kwenye vikao vyote vya maamuzi ili kuweza kuzisemea taasisi
hizo. Na kutenga bajeti kwa Maafisa habari hao ili waweze kutekeleza
majukumu yao kwa ukamilifu.
Kuhusu changamoto ya vitendea kazi Mhe. Nape alisema kuwa Wizara yake
imeanza kuwajibika kwa kuto IPad za kisasa kwa Maafisa Habari waliopo
Mikoani na katika Halmashauri za Wilaya ili ziweze kuwasaidia kutekeleza
majukumu yao kwa ufasaha, kwa mkoa wa Kagera alitoa Ipad tano kwa
Maafisa habari.
Aidha,
Mhe. Nape aliwahakikishia Waandishi wa Habari kuwa maslahi yao
yataboreshwa chini ya usimamizi wake kama Waziri mwenye dhamana ambapo
alisema kuwa Serikali ipo kwenye mchakato wa kukamilisha Mswada wa
huduma kwa vyombo vya habari ambao utazingatia mahitaji na maslahi ya
waandishi wa habari.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye kwa makini akisikiliza Hoja.
Mkurugenzi wa Radio Kasibante FM 88.5 ya Mjini Bukoba Richard Leo akitoa Mada
(Kushoto)
ni Mkurugenzi wa Radio Vision FM Ngd. Valelian na kulia ni Mr. Teso Boy
Msanii wa hapa Mjini Bukoba, Picha na Faustine Ruta, Bukoba
Mkurugenzi wa Kiroyera tours Bi Mary Kalikawe akisikiliza kwa makini.
Chief
Kalumuna(kushoto) Mea wa Mji wa Bukoba akitolea ufafanzi Jambo mbele ya
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akitoa iPad kwa ajili ya Maafisa habari
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akitolea ufafanuzi jambo
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye na Viongozi
wengine walipata nafasi wakatembelea Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba
kuona unavyoendelea.
Waziri
akipata ufafanuzi wa Umaliziaji wa Uwanja wa Kaitaba kupitia simu ya
Mkononi wakati alipotembelea Uwanja huo. Picha na Faustine Ruta, Bukoba
Sekta ya Michezo
Katika sekta ya Michezo Mhe, Nape aliwakumbusha Makatibu Tawala wa Mikoa
wao kama Wenyeviti wa kamati za michezo za mikoa kutembelea na kukaa na
viongozi wa vyama vya michezo kuwakumbusha majukumu yao na kupitia mara
kwa mara mipango kazi yao ya kazi aidha, kusimamia upatikanaji wa
viongozi wenye wajibu katika michezo na siyo vibarua wa kuingia
kuwatumikia baadhi ya watu Fulani.
Aidha, alimuagiza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba na Wenyeviti wa
Halmashauri kuhakikisha wanasimamia urudishwaji wa viwanja vilivyoporwa
na kutopitisha ramani za mipango miji zisizozingatia utengwaji wa maeneo
ya wazi ya michhezo.
Sanaa
Mhe. Nape alisema kuwa Serikali inakusudia kuirasmisha sanaa kuwa
shughuli za uchumi badala ya kuwa shughuli za burudani tu kwasababu
kwasasa sanaa inaonekana kuwa ni kuburudisha tu wakati imekuwa ikitoa
ajira kwa vijana wengi. Aidha, Serikali inakusudia kuwasimamia wasanii
kuondokana na matapeli wanaonufaika kupitia kazi zao nao kubaki hoi
hae.
Katika Sekta ya Utamaduni Mhe, Nape alisema Serikali inakusudia kutumia
utamaduni kama nyenzo ya utalii katika taifa la Tanzania
Ili kutatua changamoto zinazoikabili Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa
na Michezo zilizopo katika mikoa na Halmashauri za Wilaya Mhe. Nape
alisema Wizara yake imeanza kufanya mazungumzo na Ofisi ya Rais TAMISEMi
ili kuanzisha vitengo au idara katika Mikoa na Halmashauri za Wilaya.
Baada ya kuongera na wadau Mhe. Nape alitembelea Uwanja wa Kaitaba na
kujionea maendeleo ya ukarabati wa uwanja huo ambapo amewahakikishia
wadau wa michezo wa Mkoa wa Kagera kuwa atahakikisha anamsukuma
mkandarasi ili akamilishe uwanja huo mapema iwezekanavyo.
Sehemu
ya Uwanja wa Kaitaba ambao unaendelea kujengwa ambapo Waziri Nape
amegusia pia kuhusu umaliziaji wa Uwanja huo na kutolea ufafanuzi wa
Vifaa ambavyo vilikuwa vimekwamia bandarini na sasa vipo njiani tayari
kwa umaliziaji wa Uwanja huo.
SHARE
No comments:
Post a Comment