Jana
Julai 21 ni mwaka mmoja tangu Pierre Nkurunziza alipochaguliwa tena
kuiongoza Burundi kwa kipindi cha miaka 5, licha ya upinzani kukosowa na
kudai ya kuwa katiba ya Burundi haikumruhusu kuwania muhula wa tatu.
Utata huo
ulisababisha maandamano ya kupinga azma yake, na mauwaji ambayo Umoja
wa Mataifa unakadiria yameuwa watu zaidi ya 500. Licha ya usalama
kuonekana kurejea hatua kwa hatua kiuchumi nchi inaelezewa kuwa katika
hali ngumu kufuatia hatua ya wafadhili wakuu kusitisha misaada ya
kifedha. Changamoto kubwa zaidi hata hivyo ni kutopigwa hatua yoyote
katika majadiliano ya kisiasa yenye lengo la kumaliza mzozo unaoikabili
nchi hiyo kwa mwaka mmoja sasa.
Mwaka
mmoja tangu kufanyika uchaguzi Rais Pierre Nkurunziza na serikali yake
wameonekana kuimarika kitaifa. Waziri wa usalama Alain Guillaume Bunyoni
amesema wamefaanikiwa kupiga hatua kubwa kwa kukabiliana na walokuwa
wakiyumbisha usalama.
"Makundi
yaliyokuwa yakiendesha uhalifu, silaha zilikuwa zinamilikiwa kinyume na
sheria zimeshikwa na mamlaka ya polisi. Na bunduki za aina nyingi zaidi
ya 164,guruneti 199, na mabomu kadhaa vimekamatwa, magaidi 35
walijisalimisha mamlaka za usalama" amesema waziri Bunyoni.
Hali ikoje sasa?
Licha ya
hatua hiyo, mauwaji yakuvizia bado yame shuhudiwa, tarehe 13 mwezi huu
aliuwawa mchana kweupe Mbunge Hafsa Mossi zamani muandishi wa habari,
mwenye umaarufu kitaifa ,kikanda na kimataifa. Hadi sasa sababu za
kuuwawa kwake bado zimesalia gizani.
Halmashauri
ya Umoja wa mataifa inayo husika na haki za binaadamu imekadiria
kuuwawa kwa watu zaidi ya 500 katika kipindi cha mwaka huu mmoja.
Wakati
serikali ikionekana kuweka nguvu katika kurejesha usalama, raia
walalamika kuumia kiuchumi ambapo faranga ya Burundi yashuhudiwa
kuporomoka thamani ukilinganisha na pesa ya kigeni. Baadhi ya wananchi
wa mjini Bujumbura wanasema kuwa maisha yamezidi kuwa magumu hasa katika
masoko kwa kuwa bidhaa zinapanda bei. Hii ni baada ya wahisani wakuu
kusimamisha misaada ya kifedha.kamwe serikali haitoketi kwenye meza moja
ya majadiliano na walohusika na jaribio la kutaka kuipindua serikali
kwa sababu kwa kufanya hivyo itakuwa ni kupinga misimamo mbalimbali.
Mazungumzo ya amani
Baada ya
vikao kadha kufanyika Arusha tangu kuteuliwa Benjamin Mkapa rais
Mustaafu wa Tanzania kuwa mpatanishi bado serikali ya Burundi kupitia
waziri wa mambo ya nje Alain-Aime Nyamitwe amekumbusha kuwa kamwe
serikali haitoketi kwenye meza moja ya majadiliano na walohusika na
jaribio la kutaka kuipindua serikali kwa sababu kwa kufanya hivyo
itakuwa ni kupinga misimamo mbalimbali. Wahisani wameweka kigezo kikuu
ni kupiga hatua kwenye majadiliano jumuishi yenye dhamira ya kumaliza
mzozo huo ulozuka leo mwaka mmoja. Matarajio ya raia wa Burundi ni kuona
mgogoro huo unatafutiwa jawabu kwa wanasiasa wote kuketi chini na
kumaliza tofauti zao ili amani iweze kurejea.DW
SHARE
No comments:
Post a Comment