Ofisa
Uchumi wa Idara ya Afrika wa Nchi Zinazoendelea kutoka Geneva
(Unctad), Claudia Roethlisberger, akizungumza na wadau mbalimbali wa
masuala ya uchumi wakati wa uzinduzi wa ripoti ya maendeleo ya kiuchumi
barani Afrika iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa habari
Umoja wa Mataifa Kitengo cha Mawasiliano (UNIC),Stellah Vuzo.
Ofisa
habari Umoja wa Mataifa Kitengo cha Mawasiliano (UNIC),Stellah
Vuzo,akizungumza katika uzinduzi wa ripoti hiyo ya maendeleo ya kiuchumi
barani afrika. Kushoto ni Ofisa Uchumi wa Idara ya Afrika wa Nchi
Zinazoendelea kutoka Geneva (Unctad), Claudia Roethlisberger.
Mtafiti
wa Shirika linalojishughulisha na masuala ya utafiti wa masuala ya
uchumi (REPOA),Stephen Mwombela,akichangia mada katika mkutano huo.
Wadau mbalimbali wa masuala ya uchumi nchini wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa ripoti hiyo .
NA ELISA SHUNDA
SERIKALI
za Afrika zimeshauriwa kuchukua hatua ya kuzuia ukuaji wa madeni ya
mataifa yao ili kuepusha migogoro inayoweza kutokea kama iliyowahi
kutokea miaka ya mwishoni mwa 1980 na 1990.
Pia zimetakiwa kuongeza vyanzo vipya vya mapato kwaajili ya kugharamia maendeleo ya nchi zao.
Kauli
hiyo imetolewa jijini hapa jana na Ofisa Uchumi Idara ya Afrika,Nchi
zinazoendelea ambaye ni mwakilishi kutoka Geniva, Claudia
Reothlisberger, wakati alipokuwa akizindua Ripoti ya Maendeleo ya
Kiuchumi Barani Afrika.
“Ripoti
hii ya UNCTAD inayozinduliwa leo(jana) inayohusu Maendeleo ya Uchumi
barani Afrika, lakini tufahamu imekuwa ikichapishwa kila mwaka kuanzia
mwaka 2000,lengo likiwa ni kuzisaidia nchi za Afrika kukabiliana na
hasara ya uwezekano wa ushirikiano mkubwa wa kiuchumi na uchumi wa dunia
kwa kufanya utafiti na uchambuzi sambamba na kujenga maridhiano na
ushirikiano wa kiufundi,
“Ripoti
hii ambayo imezinduliwa chini ya Umoja wa Mataifa kuhusu Biashara na
Maendeleo (UNCTAD), inasisitiza kuwa kukopa inaweza kuwa sehemu muhimu
ya kuboresha maisha ya wananchi wa afrika lakini lazima kupata uwiano
kati ya wakati wa sasa, na baadaye kwa sababu madeni ni hatari
yanapokuwa sio endelevu” alisema.
Aidha
alisema kwa mujibu wa ripoti hiyo ilibaini kuwa angalau dola za
kimarekani bilioni 600 zinahitajika kila mwaka ili kufikia Malengo ya
Maendeleo endelevu(SDGs) barani Afrika.
Alisema
licha ya ripoti hiyo kubaini pia kwa sasa nchi nyingi za afrika zimeanza
kuondokana na utegemezi wa misaada rasmi ya maendeleo kutokana na
kutumia vyanzo vyake vipya vya fedha na vyenye ubunifu lakini zinapaswa
kuangalia vyanzo vya mapato vya nyongeza ambavyo vitasaidia afrika
kufikia malengo yake.
“Ripoti
hii ambayo pia imepewa kichwa kidogo kuwa Mienendo ya Madeni na Fedha za
maendeleo barani afrika ilionyesha kuwa zipo nchi kadhaa za Afrika
zilikopa sana katika masoko ya ndani, na nchi hizo ni Nigeria, Ghana,
Kenya,Tanzania na Zambia” alisema.
Kwa
upande wake Mchumi kutoka Benki ya Maendeleoa ya Afrika(AfDB), Prosper
Charles alisema kuwa ni wakati sasa serikali kuwa macho na hatari za
kukopa kutokana na masharti magumu yaliyopo katika kipindi hiki.
“Ili
kufikia malengo endelevu ya ya millennia ni lazima serikali ijizatiti
kutekeleza miradi yake haswa mipango yake ambayo itasaida kuondokana na
hatari ya deni la taifa”alisema.
SHARE
No comments:
Post a Comment