Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi
Kida, akitoa hotuba ya ufunguzi wa mdahalo uliolenga kujadili changamoto
zinazoikabili bajeti ya mwaka 2016/2017 kwenye sekta ya Afya na
Viwanda, kwenye makao makuu ya ESRF jijini Dar es Salaam. Mdahalo huo
umewakutanisha wasomi, wawakilishi wa Taasisi za Umma na Binafsi. (Picha
zote na K-VIS MEDIA/Khalfan Said).
TAASISI ya Utafiti ya Uchumi na Jamii (ESRF)
imewakutanisha wasomi na wawakilishi wa taasisi za umma na kibinafsi
kuchambua bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/2017 katika Sekta ya Afya na
Viwanda ili kuona inavyoweza kutatua changamoto zinazokabili Sekta hizo
kwenye mdahalo uliokutanisha wasomi, wawakilishi wa Taasisi za Umma na
Binafsi na kufanyika makao makuu ya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Akifungua
mdahalo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Dkt.Tausi Kida
alisema, Taasisi yake imeona ni vema kuwakutanisha wadau kujadili bajeti
hiyo katika sekta ya Afya na Viwanda, kwa vile zinagusa uchumi wa
wananchi.
Akiwasilisha
mada juu ya bajeti ya Serikali 2016/2017na changamoto zinazoikabili
sekta ya Afya, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Afya na Sayansi
Shirikishi, Cha Muhimbili, (MUHAS), Profesa Phares Mujinja alisema,
ingawa bajeti iliyotengwa kwenye sekta ya Afya ni kubwa, lakini bado
kuna changamoto kadhaa kwa vile Wizara hiyo imepanuka kutokana na
kuhudumia maeneo mengi.
Profesa
Mujinja alitolea mfano wa ununuzi wa madawa ambapo, zaidi ya asilimia
90 ya madawa yanayotumika huagizwa kutoka nje na hivyo fedha nyingi za
kigeni hutumika.
Katika
majumuisho yake, Profesa Mujinja alisema, ni vema Serikali ielekeze
nguvu zake kwenye uanzishwaji wa viwanda vya kuzalisha madawa na vifaa
tiba hapa nchini ili kwenda sambamba na malengo ya taifa ya maendeleo
endelevu.
Akizungumzia
kuhusu changamoto za bajeti kwenye eneo la Viwanda, muwasilisha mada
Profesa Prosper H. Ngowi kutoka Chuo Kikuu Cha Mzumbe kampasi ya Dar es
Salaam, alisema, fedha zilizotengwa kwenye Sekta ya Viwanda ni Shilingi
Bilioni 81, 871,992,000, ambapo asilimia 51 ni kwa ajili ya matumizi ya
kawaida na asilimia 49 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Kwa
mtazamo wake, Profesa Ngowi alisema, mgawanyo huo ni mzuri na sio kwa
kiwango kikubwa kwani hakuna tofauti na bajeti ya mwaka 2015/2016, na
kuonyesha wasiwasi wake muda ambao Serikali inatoa fedha hizo kuhudumia
maeneo yaliyokusudiwa.
Mhadhiri
wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), Cha
Muhimbili, Profesa Phares Mujinja, akitoa mada juu ya changamoto
zinazoikabili bajeti ya Serikali ya 2016/2017 kwenye Sekta ya Afya
wakati wa mdahalo huo.
“Bajeti
ya 2016/2017 ni Asilimia 70.3% ya ile ya 2015/2016 na kwamba wizara
hivi sasa ni kubwa kutokana na kuongezeka kwa sekta ya Uwekezaji.”
Alifafanua. (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment