Kagame amfuta kazi waziri wa afya
Rais wa Rwanda Paul Kagame amemtimua waziri wake wa afya Dr Agnes Binagwaho aliyeongoza wizara hiyo kwa kipindi cha miaka 5.
Dr
Binagwaho alikuwa miongoni mwa mawaziri vigogo katika serikali ya Rwanda
lakini wadadisi wanasema kutimuliwa kwake huenda kumetokana na utendaji
kazi usioridhisha na matatizo yanayoikumba wizara hiyo kwa sasa.
Tangazo
lililotiwa saini na waziri mkuu Anastase Murekezi limebainisha kuwa rais
wa jamhuri katika mamlaka yake amemfuta kazi waziri huyo bila kutoa
maelezo zaidi.
Lakini wadadisi wanasema huenda matatizo yaliyokuwa ndani ya wizara hiyo ndicho chanzo cha waziri huyo kutimuliwa.
Wakati wa
mkutano wa kitaifa mwezi Desemba mwaka uliopita,waziri huyo alikosolewa
vikali na washiriki waliobainisha tatizo kubwa la ugonjwa wa malaria.
Dr Binagwaho alikuwa miongoni mwa mawaziri vigogo katika serikali ya Rwanda
Takwimu zilizopo kutoka wizara ya afya zilibainisha kuwa watu zaidi ya milioni 2.5 waliathirika na ugonjwa huo mwaka jana.
Hata
hivyo katika kipindi cha miezi sita pekee ya mwaka huu wanahesabiwa
wagonjwa milioni 1.,4 idadi ambayo ni kubwa sana ikilinganishwa na miaka
5 iliyopita ambapo Rwanda ilikuwa miongoni mwa mataifa yaliyokuwa
katika nafasi nzuri ya kuangamiza ugonjwa huo.
Tatizo
lililobainishwa na wakosoaji ni uzembe uliofanywa na wizara ya afya
iliyoagiza vyandarua visivyotimiza viwango vya ubora na kugharimu wizara
hiyo dolla milioni 15 za Marekani.
Katika ripoti ya mkaguzi mkuu wa mali ya umma,wizara ya afya ilibainisha pengo la milioni 10 dollar za Marekani zilizotoweka.
Kadhalika swala la utendajikazi mbovu wa hospitali za serikali linalotokana na madaktari bingwa wanaozikimbia hospitali hizo.
wizara ya afya iliagiza vyandarua visivyotimiza viwango vya ubora na kugharimu wizara hiyo dolla milioni 15 za Marekani.
Mwezi
uliopita waziri huyo alikiri kuwepo idadi kubwa ya madaktari wanaohamia
katika hospitali binafsi wakikimbia mishahara midogo serikalini.
Kuna wanaoona kwamba maamzi yanayochukuliwa kuhusu hayaridhishi kukabiliana na matatizo hayo.
Kuhusu swala la malaria wizara ilikuwa na mkakati wa kutumia washauri wa afya ya uzazi katika kusaidia kutibu ugonjwa huo.
Aidha wizara ilikuwa na pendekezo kwamba waongezewe mshahara na kuruhusiwa kufanya kazi sehemu mbili.
Lakini mswada kuhusu hilo bado unajadiliwa bungeni.BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment