Chama
cha mchezo wa kuogelea nchini (TSA) kimeipongeza klabu ya Dar Swim Club
(DSC) kwa kufanya semina ya kuendeleza mchezo huo kwa wachezaji na
makocha iliyokuwa chini ya wakufunzi kutoka klabu ya Hamilton Aquatics
ya Dubai.
Pongezi
hizo zimetolewa na Katibu Mkuu wa TSA, Ramadhan Namkoveka mara baada ya
kutembelea mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye bwawa la kuogelea la shule
ya kimataifa ya DIA iliyopo Masaki jijini.
Mafunzo
hayo yalikuwa chini ya wakufunzi wa kimataifa wa mchezo wa kuogelea wa
klabu bingwa ya Mashariki ya Kati (Middle East) ijulikanayo kwa jina la
Hamilton Aquatics ya Dubai, Nebojsa Durkin na Katy Morris.
Mafunzo
hayo yalidhaminiwa na kampuni za Alios Finance Tanzania, Europcar, DSC,
DIA na kampuni ya utafiti na uchimbaji wa mafuta ya Maurel & Prom.
Wakufunzi
hao walifuraishwa na viwango vya waogeleaji wa klabu hiyo pamoja na
kukabiliana na changamoto mbalimbali za mchezo huo ikiwa pamoja na
kukosa bwawa la mita 50 linalotambuliwa kimataifa.
Namkoveka
alisema kuwa wamefuraishwa na mafunzo hayo ambayo yaliwahusisha
waogeleaji chipukizi (yoso) na wakubwa pia na makocha wa timu hiyo.
Alisema kuwa wamevutiwa na jinsi mafunzo hayo yalivyokuwa yanaendeshwa
na anaamini Tanzania itapata waogeleaji nyota kama wadau wa mchezo huo
wataiga mfano wa DSC.
Kocha
wa timu ya DarSwim Club, Radhia Gereza (kulia) na Salum Mapunda
(kushoto) wakiwaelekeza waogeaji watoto wa klabu ya Dar Swim Club baada
ya kupata mafunzo kutoka kwa wakufunzi wa klabu ya Hamiton Aquatics ya
Dubai.
“Nimefuraishwa
na jinsi mafunzo yalivyoendeshwa, kwa kweli nimevutiwa sana kwani
nimeona jinsi waogeleaji chipukizi waliokuwa wanaanza kujifunza mchezo,
waogeleaji wenye uelewa wa mchezo na makocha walivyokuwa wanapewa
mafunzo, hii ndiyo njia sahihi ya kuendeleza mchezo huu,”
“Naamini,
kama juhudi hizi zitaendelezwa, Tanzania itakuwa na waogeleaji wengi
wenye ubora wa kimataifa katika miaka ijayo, mchezo wetu unahitaji
sapoti kubwa sana ili kufikia malengo ambayo tumejiwekea,” alisema
Namkoveka.
Kocha wa Dar Swim Club, Michael Livingstone alisema kuwa wamepata mwanga
mkubwa katika mafunzo hayo ambayo watayatumia katika kuendeleza mchezo
katika klabu yao na kwa Taifa kwa ujumla.
“Tumejifunza
mbinu, ujuzi na mambo kadha wa kadha kuhusiana na mchezo wa kuogelea,
kwa kifupi tumepata mwanga wa hali ya juu kwa ajili ya ufundishaji kwa
waogeleaji yoso na wakubwa,” alisema.
Katibu
Mkuu wa DSC, Inviolata Itatiro amesema kuwa wamepania kuweka historia
nchini kwa kutoa waogeleaji bora na ndiyo maana waliamua kuendesha
mafunzo hayo yaliyokuwa yanafanyika kwa mara ya pili.
“Tunahitaji
sapoti katika mchezo huu, lengo ni kuona waogeleaji wanapata maendeleo
makubwa kwa kufikia viwango, nawaopongeza wadhamini Alios Finance
Tanzania, Europcar, DSC, DIA na kampuni ya utafiti na uchimbaji wa
mafuta ya Maurel & Prom kwa kutuunga mkono, gharama za kuwaleta
walimu kutoka nje ni kubwa sana,” alisema Inviolata.
Mwisho….
Mafunzo ya kuogelea siyo lazima yafanyikie kwenye maji. Hapa
mkufunzi wa kimataifa wa mchezo wa kuogelea kutoka klabu ya
Hamilton Aquatics, Nebojsa Durkin aionyesha kwa vitengo waogeleaji
wa Dar Swim Club jinsi ya kuchumpa kwenye maji (ku-dive) katika
mafunzo yaliyomalizika hivi karibuni kwenye shule ya Kimataifa ya
DIA, Masaki.
Mkufunzi wa kimataifa wa mchezo wa kuogelea kutoka klabu ya
Hamilton Aquatics ya Dubai, Nebojsa Durkin aionyesha kwa vitengo
waogeleaji wa Dar Swim Club jinsi ya kugeuka kwa kasi kwa kutumia
nguvu ya miguu katika mafunzo yaliyomalizika hivi karibuni kwenye
shule ya Kimataifa ya DIA, Masaki.
Mkufunzi wa kimataifa wa mchezo wa kuogelea kutoka klabu ya
Hamilton Aquatics ya Dubai, Katty Morris akielekeza jinsi gani ya
kuchumpa (ku-dive) kwa umbali mrefu na kwa malengo maalum kwa
waogeleaji wa Dar Swim Club katika mafunzo yaliyomalizika hivi
karibuni kwenye shule ya Kimataifa ya DIA, Masaki.
Hapa sasa ni Kazi Tu: Kocha wa Dar Swim Club, Michael
Livingstone akiwafanyika mazoezi ya kuchumpa (ku-dive) waogeleaji
wa klabu hiyo. Waogeleaji hao walifanya tendo hilo kwa staili
mbalimbali baada ya kupokea mafunzo kutoka kwa makocha wa klabu
maarufu ya Hamilton Aquatics, Nebojsa Durkin na Katy Morris.
Kocha wa Dar Swim Club, Salum Mapunda akiwasimamia waogeaji
yoso wa klabu ya hiyo katika mafunzo hayo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Kuogelea (TSA) Ramadhan Namkoveka (wa
tatu kutoka kushoto) na Mkurugenzi wa Ufundi Amina Mfaume (wa tatu
kutokakulia) wakiwa ktika picha ya pamoja na wakufunzi wa mchezo
huo kutoka Dubai, Nebojsa Durkin (wa pili kushoto), Katy Morris (wa
nne kutoka kushoto) na viongozi na makocha na viongozi wa klabu
maarufu ya Dar Swim Club, Kocha Kanisi Mabena (wa kwanza kushoto),
Michael Livingstone (wa pili kulia) na Katibu Mkuu wa klabu hiyo
Inviolata "Iron Lady" Itatiro wa kwanza kulia.
SHARE
No comments:
Post a Comment