Rais wa
Uturuki, Recep Tayyip Erdogan ametangaza hali ya hatari itakayodumu kwa
miezi mitatu ili kutoa nafasi kwa mamlaka kuchukua hatua stahiki dhidi
ya wanaoshukiwa kushiriki mapinduzi ya kijeshi yaliyoshindwa juma
lililopita.
Erdogan,
ambaye alianzisha hatua ya kamata kamata katika taasisi mbalimbali tangu
baada ya mapinduzi yaliyoshindwa, amesema hatua hiyo inazingatia katiba
ya Uturuki na hajakiuka utawala wa sheria wala uhuru wa raia wa
Uturuki.
Hali ya
hatari, ambayo itaanza kutekelezwa mara tu baada ya kuchapishwa kwenye
Gazeti la Serikali , itamruhusu Rais na Baraza kufanya kazi za bunge
kupitisha sheria mpya na kuweka na kuweka mipaka au kusimamisha kwa muda
baadhi ya haki na uhuru wa raia inapolazimika kufanya hivyo.
Erdogan
alitoa tangazo hilo akiwa kwenye matangazo ya moja kwa moja kwa njia ya
Televisheni mbele ya mawaziri wa Serikali baada ya mkutano wa baraza la
usalama la Taifa.
Katika
hatua nyingine, Majerali wa jeshi wameshtakiwa rasmi wakihusishwa na
mapinduzi ya juma lililopita, pia imetangazwa kuwa majaji wa kijeshi na
waendesha mashtaka wanafanyiwa uchunguzi.
Halikadhalika
mamia ya shule na taasisi za kielimu zimefungwa.waalimu na wana taaluma
ni sehemu ya maelfu ya wanajeshi, wafanya kazi wa umma na wengine
wanaoshukiwa kuiangusha serikali, mpango unaodaiwa kuongozwa na Kiongozi
wa Kidini aishie uhamishoni nchini Marekani, Fethullah Gulen.
Wanafunzi hawa wanaeleza hatua hii ina maana gani kwa mustakabali wa maisha yao.BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment