Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia)
akipokea zawadi ya bango la picha zilizopigwa na baadhi ya Waandishi wa
Habari waliowahi kujengewa uwezo na Tanzania Media Foundation toka kwa
Mkufunzi wa Picha, Bw. Mwanzo Millinga 12 Julai, 2016 jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye
(kushoto) akipokea bahasha yenye mafanikio ya Tanzania Media Foundation
ambayo yamefanywa nchini katika kuwajengea uwezo Waandishi wa habari
toka kwa Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation, Bw. Ernest Sungura 12
Julai, 2016 jjijjini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiongea na wageni waalikwa pamoja na baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhuria hafla ya unzinduzi wa Miradi Nane inayofadhiliwa na Tanzania Media Foundation 12 Julai, 2016 jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wageni waalikwa pamoja na waandshi wa habari wakifuatilia hafla ya Uzinduzi wa Miradi nane inayodhaminiwa na Tanzania Media Foundation 12 Julai, 2016 jijini Dar es Salaam.
(Picha/Stori na Benedict Liwenga)
Serikali kwa kushirikiana na Uongozi wa Tanzania Media Foundation itaendelea kushirikiana bega kwa bega katika kuwawezesha Waandishi wa Habari nchini kupenda kutembelea maeneo ya vijijini na kuandika habari mbalimbali kuhusu changamoto za maeneo hayo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiongea na wageni waalikwa pamoja na baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhuria hafla ya unzinduzi wa Miradi Nane inayofadhiliwa na Tanzania Media Foundation 12 Julai, 2016 jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wageni waalikwa pamoja na waandshi wa habari wakifuatilia hafla ya Uzinduzi wa Miradi nane inayodhaminiwa na Tanzania Media Foundation 12 Julai, 2016 jijini Dar es Salaam.
(Picha/Stori na Benedict Liwenga)
Serikali kwa kushirikiana na Uongozi wa Tanzania Media Foundation itaendelea kushirikiana bega kwa bega katika kuwawezesha Waandishi wa Habari nchini kupenda kutembelea maeneo ya vijijini na kuandika habari mbalimbali kuhusu changamoto za maeneo hayo.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Mhe. Nape Nnauye wakati akizindua Miradi Nane ambayo inafadhiliwa na
Taasisi hiyo ambayo unahusisha Waaandishi wa Habari kutembelea maeneo ya
vijijini na kuandika habari mbalimbali kwa lengo la kuelimisha Umma.
Mhe.
Nnauye amesema kuwa, Serikali inatambua mchango mkubwa unaofanywa na
Taasisi hiyo ya kuwajengea uwezo Waandishi wa habari na kuwawezesha
kifedha kwa ajili ya kwenda kutafuta habari mbalimbali katika maeneo ya
vijijini.
‘’Ni
muhimu kwa waandishi wa habari kufika maeneo ya vijijini na kuapata
habari mbalimbali kwa jili ya kuhabarisha umma, hivyo Serikali bado iko
na nyie na itaendelea kuwaunga mkono na endeleeni na kazi hiyo nzuri’’,
alisema Mhe. Nnauye.
Ameongeza
kuwa, kuna haja ya Taasisi hiyo kuendelea kujenga uwezo wa kusaidia
kupata umakini katika kazi za habari ili jamii iweze kuwa na imani na
Serikali pamoja na Vyombo vya habari na pia kuonyesha juhudi ya
kuendelea kuwajengea uwezo wanahabari ili waweze kuwafikia watu wenye
mahitaji makubwa ya habari ambao ni watu wa vijijjini ambao wakati
mwingi wamekuwa wakichelewa kupata habari.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation, Bw. Ernest Sungura
ameyataja baadhi ya mafanikio yaliyofikiwa na Taasisi hiyo katika
kuwajengea uwezo wanahabari nchini ambapo amesema kuwa, mpaka sasa
wameweza kuwajengea uwezo jumla ya Waandishi wa habari wapatao 700
pamoja na Vyombo vya Habari 135.
Mbali
na kuanza na miradi ya mwandishi mmoja mmoja, kwa sasa wanatarajia
kuanza na miradi mingine inayoanza mwishoni mwa mwezi huu na itakuwa ni
ya Awamu ya Pili ambapo itahusisha jumla ya Waandishi wa habari wapatao
30 kwenda vijijini kufanya kazi za kihabari na kupewa mafunzo ya namna
ya kuandika habari za vijijini.
‘’Kwa
sasa tumeanza mradi wa watu kubobea katika eneo maalum na safari hii
tutajikita katika masuala ya Viwanda yaani kuwaandaa waandishi wa habari
watakaobobea katika masuala ya viwanda na tayari tumeshamdokeza Waziri
wa Viwanda kuhusu taarifa hizo kwa ajili ya kuizindua miradi hiyo’’,
alisema Sungura.
Ameongeza
kuwa katika kuandika masuala ya viwanda, tayari kuna waandishi wa
habari wapatao 10 ambao hivi sasa wanajengewa uwezo ili waweze kuendana
na kasi ya Serikali na katika suala la kuwandaa waandishi hao wanatumia
Waandishi wa habari wazoefu pamoja na wadau wengine.
Amefafanua
kuwa, lengo kubwa la kazi hizo zote ni kuwawezesha waandishi nchini
kuweza kuyafikia maeneo ambayo yamekuwa hayafikiki, hivyo wanatoa
rasimali fedha kwa waandshi hao ili kuweza kutembelea maeneo hayo na
kuhabarisha umma.
‘’Ziko
takwimu nyingi kila mahali kama vile za maji, afya, alimu lakini baadhi
ya waandishi wetu hawafanyi ule uandishi wa kuzifanya takwimu hizo
zieleweke na ziwe na manufaa kwa walaji, hivyo sisi tumeamua kuwajengea
waandishi katika maeneo hayo’’, alisema Sungura.
SHARE
No comments:
Post a Comment