TRA

TRA

Wednesday, August 31, 2016

Ali Bongo atangazwa mshindi wa uchaguzi Gabon

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Ali Bongo atangazwa mshindi wa uchaguzi nchini Bongo
Ali Bongo atangazwa mshindi wa uchaguzi nchini Bongo
Wanachama wa tume ya Uchaguzi mkuu nchini Gabon wametangaza kuwa rais Ali Bongo, amehifadhi kiti chake cha urais baada ya kumshinda mpinzani wake Jean Ping.
Ushindi huo ni baada ya kumalizika kwa shughuli za upigaji kura, hapo siku ya Jumamosi.
Lakini mwaandishi wa habari wa BBC mjini Libreville, amesema kuwa wajumbe wanaowakilisha upinzani katika tume ya uchaguzi, wameondoka ndani ya ukumbi wa kuhesabu na kusawazisha matokeo ya kura, na kukataa kutia saini hati zinazompa ushindi rais Bongo.
Walinda usalama wanapiga doria katika barabara za mji mkuu Libreville huku taharuki ikitanda kote nchini humo.
Familia ya Bongo imetawala Gabon kwa nusu karne huku Omar Bongo akitawala kwa miongo minne, na mwanawe rais wa sasa Ali, alichukua hatamu za uongozi mnamo mwaka wa 2009.BBC

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger