
Kansela
Angela Merkel wa Ujerumani amekiri kumefanyika makosa Ujerumani na Umoja
wa Ulaya katika suala la mzozo wa wakimbizi lakini amesisitiza kwamba
Ujerumani haitabadilika na itaendelea kubakia kama Ujerumani.
Merkel
alisema kwamba ni wazi kabisa Ujerumani ni nchi madhubuti na dhamira yeo
inapaswa kuwa tayari wameweza kumudu mambo mengi kwa hiyo wanaweza
kumudu suala la wakimbizi na iwapo watakuwa na vizingiti njiani hawana
budi kuvishinda na nchi itafanya kila iwezalo kwa kushirikiana na
serikali za majimbo kufanikisha jambo hilo.
Ilikuwa
ni tarehe 31 mwezi wa Augusti mwaka 2015 wakati Kansela Angela alipotowa
kauli yake hiyo mashuhuri "wir schaffen das" tutalimudu hili wakati
Ujerumani ilipowakaribisha mamia kwa maelfu ya wakimbizi na wahamiaji
nchini waliokuwa wakikimbia vita na mizozo nchini mwao.
Akizungumza
katika mahojiano na gazeti la Ujerumani la Sueddeutsche Zeitung
yaliyochapishwa leo juu ya kauli mbiu yake hiyo ambayo imewagawa
wananchi wa Ujerumani kimtizamo Merkel amesisitiza kwamba inaendelea
kubakia kiini sahihi kwa jukumu la kukabiliana na mzozo huo.
Kansela
Merkel ambaye kwa miezi kadhaa alikabiliwa na shutuma kwa kuonyesha moyo
huo wa kujiamini kwa matumaini katika kuwashughulikia wakimbizi
ameliambia gazeti hilo la Ujerumani kwamba Ujerumani na mataifa mengine
ya Umoja wa Ulaya yalishindwa kuchukuwa hatua licha ya kuwepo kwa
ushahidi ya mzozo huo kuzidi kuwa mkubwa.
Makosa yamefanyika
Merkerl
amesema kuna masuala ya kisiasa ambayo mtu anaweza kuyaona kuwa yanakuja
lakini kwa wakati fulani hayawaingii watu akilini na nchini Ujerumani
wamelipuuza tatizo hilo kwa muda mrefu halikadhalika kuzuwiya hata na
haja ya kutafutafuta usuluhishi wa umajumui wa Ulaya. Ameongeza kusema
kwamba Ujerumani kwa miaka kadhaa imekuwa pia ikifanya makosa kwa
kupinga mpango wa kugawana wakimbizi kwa uwiano na kulitupia jukumu hilo
idara ya mipaka ya majini ya Umoja wa Ulaya.
Merkel
amesema wakimbizi wengi walikuja mwaka 2004 na mwaka 2005 na
wakaiwachilia Uhispania na wengine wa Idara ya Umoja wa Ulaya ya masuala
ya mipaka ya nje kuwashughulikia. Amesema Ujerumani ilikuwa na furaha
sana kwamba baada ya kupokea wakimbizi wengi wakati wa vita nchini
Yugoslavia nchi nyengine sasa zilikuwa zinastahiki kulishughulikia suala
hilo amesema jambo hilo hawezi kulikanusha.
Katika mahojiano hayo Merkel pia amekaririwa akisema "Ujerumani itabakia kuwa Ujerumani ikiwa na kila kitu ambacho inakipenda "
Ameongeza
kusema mabadiliko yamekuwa yakitokea kwa miongo mingi lakini mabadiliko
sio kitu kibaya yanahitajika katika maisha jambo lililo wazi ni kwamba
Ujerumani haitoyaacha maadili yake.
Ugaidi hauletwi na wakimbizi
Kansela
Merkel pia ameyatumia mahojiano hayo kuwashutumu wanasiasa wa Ujerumani
kwa kuwataka wasitumie lugha kali na wasishiriki kupalilia kauli kwamba
vitisho vinatoka nje.
Merkel ni
"wazi sio sahihi kwamba ugaidi unaletwa na wakimbizi " na kwamba "
tayari ulikuwepo hapa katika aina mbali mbali na kwamba wanaotaka
kufanya mashambulizi wamekuwa wakisubiri kufanya hivyo."
Merkel na
Halmashauri ya Umoja wa Ulaya wameshindwa kupiga hatua kubwa katika
juhudi za kuyashirikisha mataiafa mengine ya Umoja wa Ulaya kugawana
mzigo wa wakimbizi wanaowasili hivi sasa. DW
SHARE








No comments:
Post a Comment