Makamu mpya wa rais wa Sudan Kusini Taban Deng Gai
Makamo wa
raisi mpya wa Sudani Kusini Taban Deng Gai ameanza ziara ya siku mbili
mjini Khartoum kujadili masuala nyeti ambayo bado hayakufanyiwa kazi
tangu Sudan kaskazini kujitenga na kusini mwaka 2011.
Ziara hii
ya kwanza ya Deng nchini sudan akiwa makamo wa raisi inakuja makuma
kadhaa baada ya kuteuliwa kushika nafasi ya aliyekuwa kiongozi wa waasi
Riek Machar kufuatia ghasia zilizoibuka mjini Juba na kusababisha vifo
vya mamia ya watu mnamo mwezi Julai.
Waziri wa
mambo ya kigeni wa sudan kaskazini Kamal Ismail amesema kuwa wamempokea
Taban Deng kama makamo wa kwanza wa raisi wa taifa la Sudan Kusini.
Wakati
Khartoum ikionesha kumtambua Deng kama makamo wa raisi wa sudan kusini
mataifa nane yanayounda kanda la IGAD ambayo pia Sudan ni mwanachama
bado kutambua uteuzi wake.
Masuala
ambayo hayajapatiwa ufumbuzi tangu kujitenga kwa Sudani Kusini ni pamoja
na hadhi ya wilaya ya mpakani ya Abyei iliyochukuliwa na Khartoum,
ambayo imekuwa ikitakiwa kupiga kura kuhusu hatma yake na malipo ambayo
Juba inapaswa kufanya kwa kutumia bomba la mafuta kusafirisha mafuta
nchini Sudan.RFI
SHARE
No comments:
Post a Comment