
Mkuu wa
mkoa wa Arusha,Mheshimiwa Mrisho Gambo(katikati)akizungumza na Askofu wa
Kanisa la Anglikan,Dayosisi ya Mount Kilimanjaro,Stanley Hotay(kushoto) alipomtembelea ofisini kwake

Askofu wa Kanisa la Anglikan,Dayosisi ya Mount Kilimanjaro,Stanley Hotay(kushoto) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mh.Mrisho Gambo.

Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mheshimiwa Mrisho Gambo akiagana na Askofu wa Kanisa la Anglikan Dayosisi ya Mount Kilimanjaro,Stanley Hotay(kulia) baada ya mazungumzo yao.
Nteghenjwa Hosseah – Arusha
Mkuu
wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo ameendelea na ziara yake ya
kujitambulisha kwa viongozi wa dini ukiwa ni utaratibu aliojiwekea wa
kukutana na viongozi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo hivi
karibuni.
Mh.Gambo
amekutana na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania(KKKT)Dayosisi ya Kaskazini Kati,Mchungaji Solomon
Masangwa , Askofu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God(EAGT)
mkoa wa Arusha,Leonard Mwizarubi na Askofu Stanley Hotay wa Kanisa la
Anglikana , Dayosisi ya Mount
Kilimanjaro.
Kilimanjaro.
Katika
mazungumzo na viongozi hao kwa nyakati tofauti mbali na kujitambulisha
aliwahakikisha dhamira ya serikali kulinda na kuheshimu uhuru na haki ya
kuabudu ambayo imekuwepo nchini kwa muda mrefu ikiwa ni njia ya kuwa na
taifa la watu wenye hofu ya Mungu.
Alisema kutokana na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dr. John Joseph Magufuli
kutaka kuwainua wananchi wa chini kupitia mapato ya ndani halmashauri
zimetenga asilimia 10 kutoka kwenye mapato hayo kwa ajili ya mikopo
yenye riba nafuu kwa Wanawake na Vijana wajasiriamali zitakazowawezesha
kufanya shughuli za uzalishaji mali.
Amewataka wawajulishe waumini wa dini zote na serikali iko tayarikupanga utaratibu wa maafisa maendeleo ya Jamii na Vijana kupita na kutoa elimu
kwa makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na madhehebu ya dini hili iwe
inufaishe watu wote katika mkoa huu bila kujali itikadi za kidini wala
kisiasa.
Askofu
Stanley Hotay aliupongeza uongozi wa mkoa kuimarisha hali ya utulivu na
kuomba vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo Mkuu wa mkoa ndiye
Mwenyekiti wake kukabiliana na changamoto za kiusalama na viashiria vya
uvunjifu wa amani.
Aidha alishauri kutokana
na idadi ya watu wanaotumia usafiri wa anga kuongezeka kuna haja ya
Serikali kufikiria uwezekano wa kupanua zaidi uwanja wa ndege wa Arusha
uliopo Kisongo ili uweze kukidhi mahitaji ya sasa badala ya kutegemea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) pekee.
Mh.
Gambo amewahakikishia viongozi hao kuwa serikali itakua ikiwashirikisha
mipango mbalimbali inayokusudia kuitekeleza ili watoe mawazo yao
katika kuiboresha na kuifanya itekelezeke kwa wepesi zaidi.(P.T)
SHARE








No comments:
Post a Comment