
Mkurugenzi
wa Mikataba, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi. Eveline
Makala akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa nafunzo (hawapo
pichani)

Washiriki
wa mafunzo wakifuatilia Mada ya dhana ya ubia iliyokuwa
ikiwasilishwa na Dkt Frank Mshiru kutoka Wizara ya Fedha na Uchumi
Na Mwandishi wetu
Serikali
ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania imeendelea kuwajengea uwezo
watendaji wake ili kuwawezesha kuhakiki na kusimamia utekelezwaji wa
miradi ya uwekezaji ya ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi
(Public Private Partnership) katika sekta ya Nishati na madini.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa watendaji mbalimbali wa Serikali
yanayofanyika kuanzia Agosti 1-4,2016 mkoani Tanga, Naibu Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Ndugu Gerson Mdemu ameeleza kuwa Serikali imechukua
hatua hiyo ili kuondoa ombwe la uelewa wa watumishi wa umma kuhusu
Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi ya mwaka 2010
(The Public Private Partnership Act).
Itakumbukwa
kuwa, kabla ya mwaka 2010,hakukuwa na Sheria iliyosimamia huduma
itolewayo na ubia kati ya Sekta ya umma na Sekta binafsi ingawa tayari
kulikuwa na huduma ambazo zilikuwa zikitolewa kwa sura ya ubia kati ya
mashirika ya dini na serikali au mashirika ya umma katika sekta ya
afya,elimu na maji jambo ambalo lilipelekea Serikali kutumia gharama
kubwa katika kuhakikisha kuwa miradi husika inatekelezwa ipasavyo.
Ili
kuondokana na changamoto hiyo, Serikali ililazimika kurasimisha shughuli
zilizokuwa zikifanywa na sekta binafsi katika utoaji wa huduma kwa umma
kwa kutunga Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya umma na sekta binafsi kwa
lengo la kutumia teknolojia na utaalamu wa sekta binafsi kutoa huduma
yenye gharama nafuu kwa umma na kuhakikisha kuwa huduma inayotolewa na
sekta binafsi inaendana na vigezo vilivyowekwa na Serikali.
Aidha
Ndugu Mdemu alifafanua kuwa Sheria hii imeipa Sekta binafsi njia mbili
za utoaji huduma ambazo ni mosi, kujenga miundombinu mipya na bora na
pili ni kumiliki miundombinu ya Serikali, kuiboresha na kuiendesha
wakati wa kutoa huduma bora na kuikabidhi Serikalini baada ya muda wa
mkataba kukamilika.
Vilevile
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ametumia fursa hiyo kuzikumbusha
taasisi za Serikali kuzingatia ushauri wa kisheria unaotolewa na Ofisi
ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika utekelezaji wa mikataba na
majukumu mbalimbali kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 23 cha Sheria
ya Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya
mwaka 2005 (The Attorney General [Discharge of Duties] Act) ambacho
kinaeleza kuwa ushauri unaotolewa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali ndio msimamo wa Serikali hadi utakapoondolewa na Mwanasheria
Mkuu wa Serikali mwenyewe au Mahakama.
“Kwa
Mawakili wa Serikali,umuhimu wenu unatokana na nafasi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali kama ilivyowekwa wazi Kikatiba. Mwanasheria yeyote wa
Wizara,Taasisi,Mashirika ya Umma au Serikali za mitaa anayetoa ushauri
wa kisheria katika eneo lake la kazi,kimsingi anafanya kazi kwa niaba ya
Mwanasheria Mkuu” aliongeza Ndugu Mdemu.
Naye
Mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Dkt Mhiru
alieleza kuwa washiriki watajengewa uwezo wa masuala muhimu ya
kuzingatia wakati wa kuhakiki mikataba ya ubia kati ya sekta ya umma na
sekta binafsi ili kuiwezesha nchi kupiga hatua katika ukuaji wa uchumi .
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Mikataba kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali,Bi Evelyne Makala alieleza kuwa sekta ya Nishati ni sekta
ambayo ina mikataba mingi ya ubia na yenye maslahi makubwa kwa Taifa
hivyo mafunzo haya yatasaidia katika kutoa mwongozo wa uhakiki na
kusimamia miradi ya uwekezaji katika sekta ya Nishati na madini.
Mafunzo
hayo amabayo yamefadhiliwa na Shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa
(UNDP) yameshirikikisha watendaji wa Serikali kutoka Ofisi ya Waziri
Mkuu,Wizara ya Nishati na Madini,Wizara ya Fedha na Mipango,Wizara ya
Mambo ya Nje,Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kimataifa, Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Shirika la Maendeleo la Taifa
(NDC), Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Wakala wa Barabara Tanzania
(TANROADS), Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Zanzibar,Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa Jamhuri ya Muungano,na watumishi kutoka
Ofisi za Mwanasheria Mkuu za Mikoa ya Pwani,Arusha,Morogoro,Tanga na
Ofisi ya Wilaya ya Monduli. (P.
SHARE
No comments:
Post a Comment