Wizara
ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar pamoja imewahasa wazazi
nchini wametakiwa kutoa uhuru kwa watoto wao wa kike kucheza mpira wa
miguu ili kuifikisha nchi katika ushindi na kuitangaza Kimataifa.
Hayo
yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na
Michezo Zanzibar Hassan Mitawi alipokuwa akifungua mashindano ya Airtel
Rising Stars yaliyofanyika uwanja wa Amaan.
Alisema
bila ya michezo Zanzibar haiwezi kujulikana hivyo ni vyema kwa wazazi
na walezi kuwapa motisha watoto wao wa kike kushiriki katika michezo
hasa mpira wa miguu.
Alisema
mchezo wa mpira wa miguu ni mchezo wenye kutoa ajira kama ilivyo kwa
wanaume lakini tabia ya baadhi ya wazazi kuwakataza watoto wao wa kike
kujiingiza katika soka kuwakosesha fursa zinazotokana na mpira ikiwemo
afya bora, ajira pamoja na kuchangia katika kukuza soka la wanawake
nchini.
Mitawi
alisema watu wanazaliwa na vipaji na vipaji hivyo vinapaswa kuendelezwa
hasa kwa upande wa Zanzibar wanawake washirikiane kudumisha michezo.
Aidha
aliishukuru Airtel kuzidi kukuza na kusaidia michezo nchini na kuwataka
kuendelea kuwekeza katika michezo hususani soka la wanawake.
Awali
Mwenyekiti wa soka la wanawake Hatima Mwalimu alisema mashindano hayo
yatasaidia kuinua vipaji vitakavyoisaidia Zanzibar kushiriki katika
mashindano mbalimbali.
Nae
Meneja Mauzo wa Airtel Zanzibar Muhidin Mikadadi alisema “Tunajisikia
fahari kusaidia mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 hapa
nchini na tumejipanga kuibua vipaji vya vijana kupitia program hii.
Tunafurahi kuona vijana wengi wanajitokeza kushiriki mashindano hayo na
tunawashukuru ZFA na Wizara ya Michezo kuwaunga mkono katika kusaidia na
kukuza michezo nchini”.
Huu ni
msimu wa sita kwa mashindano ya Airtel Rising Star nchini kwa mwaka
humu Zanzibar impeta nafasi ya kushiriki, jumla ya timu sita
zinashiriki katika mashindano haya ni pamoja na Mwenge kutoka Wilaya
ya Kusini, Kidimni Kutoka Wilaya ya Kati,New Generation Kutoka Mkoa wa
Mjini Magharibi, Jumbi Women kutoka Wilaya ya Kati na Bungi Sisters
kutoka Wilaya ya Kati.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utalii, Utamanduni na Michezo Zanzibar
Hassan Mitawi akikangua timu wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel
Rising Stars Zanzibar Ijumaa 5 Agosti 2016.
Mchezaji
wa Bungi Sister FC Agatha Peter (nyekundu) akichuana na beki wa Jumbi
Woman Fighter Arafa Mbaraka wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel
Rising Stars Zanzibar. Bungi FC ilishinda 3-0.
Mchezaji
wa Bungi Sister FC Swahiba Khamis (nyekundi) akichuana na Shamira
Shaban wa Jumbi Woman wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel Rising
Stars Zanzibar. Bungi FC ilishinda 3-0.
Mchezaji
wa Bungi FC Suzan Francis (nyekundu) akichuana na Agnes Andrew wa Jumbi
Woman Fighter wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel Rising Stars
Zanzibar. Bungi FC ilishinda 3-0.
Mchezaji
wa Bungi FC Suzan Francis (nyekundu) akichuana na Agnes Andrew wa Jumbi
Woman Fighter wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel Rising Stars
Zanzibar. Bungi FC ilishinda 3-0.
Jumbi
Woman fighter FC defender Agnes Adrew (white) runs past Bungi FC player
striker Suzan Fransi (red) during the launch of Airtel Rising Stars 2016
Zanzibar. Bungi Sister won 3-0.
Mchezaji
wa Bungi FC Suzan Francis (nyekundu) akichuana na Agnes Andrew wakati
wa uzinduzi wa michuano ya Airtel Rising Stars Zanzibar. Bungi FC
ilishinda 3-0.
Mchezaji
wa Bungi Agatha Peter akichuana na Swahiba Hamis wakati wa uzinduzi wa
michuano ya Airtel Rising Stars Zanzibar. Bungi FC ilishinda 3-0.
Mchezaji
wa Bungi Juba Skampunda akichuana na Semeni Hamad wakati wa uzinduzi wa
michuano ya Airtel Rising Stars Zanzibar. Bungi FC ilishinda 3-0.
SHARE
No comments:
Post a Comment