WAZIRI
wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba ameagiza uongozi wa
Magereza ya mkoa wa Iringa kuanza mchakato wa kuhamisha magereza
ya Manispaa ya Iringa ili eneo hilo kutumika kupanua Hospitali ya
rufaa ya mkoa wa Iringa.
Nchemba
ametoa agizo hilo leo baada ya kutembelea eneo hilo ambalo
limekuwa likiombwa kwa muda mrefu na viongozi wa serikali ya mkoa
wa Iringa ili litumike kwa ajili ya matumizi ya Hospitali hiyo ya
Rufaa ya mkoa wa Iringa .
Akizungumza
baada ya kutembelea eneo la Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa
alisema kuwa amekubaliana na maombi ya viongozi wa mkoa wa Iringa ya
kuomba gereza hilo kuhamishiwa katika eneo la Mlolo nje kidogo
na Manispaa ya Iringa huku eneo hilo la Magereza litumike kupanua
majengo ya Hospitali hiyo ya Rufaa ya mkoa wa Iringa.
“
Kwa kawaida kati ya Hospitali na magereza kinachotakiwa kuwepo
mjini ni Hospitali na sio magereza hivyo hivyo kati ya mgonjwa na
mfungwa ama mahabusu anayeweza kufanya kazi ya kufyatua tofari za
ujenzi ni mahabusu ama mfungwa na sio mgonjwa , hivyo naagiza mtaalam
wa ujenzi wa magereza kuanza kuandaa vifaa vya kufyatualia tofari
na kwa kufuata taratibu za magereza waorodheshwe wale ambao watakuwa
tayari kujitolea kufanya kazi ya ujenzi ili kazi hiyo ianze”
Hata
hivyo waziri huyo alisema kuwa kuanzia leo anataka kupata orodha
ya wafungwa waliopo gerezani hapo ambao wanauwezo wa kufanya kazi.
Pia
alisema suala la kuhamishwa kwa gereza hilo litafanyika kwa awamu
na kuwa wakati gereza linajengwa na baadhi ya nyumba za watumishi
bado askari wataendelea kuishi katika eneo hilo huku majengo yao
likiwemo jengo la Ghorofa utawekwa utaratibu wa kujengewa jingine
ili hilo linalotumiwa na magereza litumike kwa ajili ya madaktari.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akisalimiana na Waziri wa
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi (kulia) baada ya kukutana
katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, leo.
Waziri
wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi (katikati)
akimtambulisha Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela kwa Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, wakati walipokutana leo nje
ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akisalimiana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, SACP Peter Kakamba.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akizungumza katika kikao na Uongozi wa Mkoa wa Iringa.
Mbunge
wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa wa pili kushoto wakisalimiana
kwa furaha na mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abeid Kiponza huku Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba na Mkuu wa Wilaya ya Iringa,
Richard Kasesela (kushoto) wakiangua kicheko
Mganga
mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Salmu Robart akimwonyesha waziri Nchemba
ufinyu wa eneo la Hospitali hiyo ya rufaa ya mkoa wa Iringa. Picha
na MatukiodaimaBlog.
SHARE
No comments:
Post a Comment