Kiongozi
Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Kabwe Zitto (katikati), akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana asubuhi, wakati
akitoa tamko la kamati kuu ya chama hicho baada ya kufanyika kikao
chake cha kawaida jana. Kushoto ni Kaimu Katibu mkuu wa chama hicho,
Juma Sanani na kulia ni Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara, Shaban Mambo.
Taswira
meza kuu. Kutoka kushoto ni Kaimu Katibu mkuu wa chama hicho, Juma
Sanani , Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Kabwe Zitto, Makamu Mwenyekiti wa
chama hicho Tanzania Bara, Shaban Mambo, Makamu Mwenyekiti Tanzania
Zanzibar, Ramadhan Ramadhan na Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara, Msafiri
Mtemelwa.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
CHAMA Cha
ACT Wazalendo kimesema katika kipindi cha miezi 6 tu ya kwanza ya
utawala wa Rais Dk. John Magufuli uchumi wa nchi umepungua hadi kufikia
asilimia nne ukilinganisha na vipindi vingine vilivyopita.
Hayo
yamebainishwa na Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Kabwe Zitto Dar es Salaam
leo wakati akitoa tamko la kamati kuu ya chama hicho kuhusu hali ya
nchi baada ya kikao cha kawaida kilichofanyika jana.
Kabwe
alisema katika miaka 10-15 iliyopita, nchi yetu imejenga uchumi ambao
umekuwa ukikua kwa kiwango cha asilimia 6-7 kwa mwaka katika kipindi
chote hiki. Ukuaji huu wa uchumi ulitokana na juhudi za nchi katika
kuvutia wawekezaji na kuchochea shughuli za uzalishaji mali kwa wananchi
wenye kipato cha chini.
Alisema
awamu ya tano ya Serikali ya Chama cha Mapinduzi imerithi changamoto ya
uchumi unaokua bila kuwafaidisha wananchi wa kawaida. Hili ndilo
tulitegemea Serikali mpya ishughulike nalo.
” Kamati
kuu yetu imeshtushwa na hali ya kuanza kudorora kwa shughuli za uchumi
katika kipindi cha miezi kumi ya utawala wa awamu ya tano” alisema Kabwe
Akitolea
mafano alisema taarifa za Benki Kuu zilizopo kwenye tovuti yake
(Quarterly Economic Review na Monthly Economic Review) kwa robo ya
mwisho ya mwaka 2015 (Oktoba?- Desemba 2015) zinaonesha kuwa kasi ya
ukuaji wa Pato la Taifa ilikuwa 9%. Katika robo ya kwanza ya mwaka 2016
(Januari – Machi 2016) kasi ya ukuaji wa Pato la Taifa ilishuka hadi
kufikia 5.5%. Kiuchumi, hii inamaanisha kuwa ukuaji wa shughuli za
kiuchumi katika kipindi cha miezi 6 ya mwanzo ya utawala wa awamu ya
tano chini ya Rais Magufuli umepungua kwa 4%!?
Alisema
shughuli za uchumi zinazohusu wananchi masikini zimeshuka kutoka kasi ya
ukuaji ya 10.20% katika robo ya mwisho ya mwaka 2015 mpaka 2.7% katika
robo ya kwanza ya mwaka 2016, ikiwa ni punguzo la 8% ndani ya kipindi
kisichozidi miezi sita. Hii inamaanisha kwamba Wananchi wetu wanazidi
kudumbukia kwenye ufukara kwa kasi tangu awamu ya tano ya Serikali ya
Chama Mapinduzi iingie madarakani.
Aliongeza
kuwa ukuaji wa sekta ya ujenzi katika robo ya mwisho ya mwaka 2015
ulikuwa ni 13.8% lakini ukuaji wa sekta hiyo katika robo ya kwanza ya
mwaka 2016 ilikuwa ni 4.30%, ikiwa ni tofauti ya takribani -10%. Hii ni
kwa sababu uwekezaji katika sekta hii umeanza kushuka.
“Kasi ya
ukuaji wa sekta ya usafirishaji imeporomoka kutoka kukua kwa 14.50% robo
ya mwisho ya 2015 mpaka kukua kwa 7.9% robo ya kwanza ya 2016, ikiwa ni
kuporoka kwa 7% katika kipindi cha miezi 6 tu ya kwanza ya utawala wa
Rais Magufuli. Kuporomoka kwa sekta ya usafirishaji itaathiri watu
wengi, wakiwemo madereva, matingo, pamoja na mama ntilie wanaowauzia
chakula” alisema .
Alisema
kwa kuzingatia mwenendo wa hali ya uchumi katika nchi, kaamati kuu ya
chama hicho wanaitaka serikali izingatie ‘’sayansi ya uchumi’’ katika
kuendesha uchumi wa nchi. Uamuzi wa CCM wa kuitelekeza serikali yake kwa
mwanasiasa mmoja anayedhani ndiye anayejua kila kitu na yeye kugeuka
kuwa mshauri wa washauri wa uchumi badala ya washauri wa uchumi
kumshauri yeye, itasambaratisha uwekezaji nchini na kuua kabisa juhudi
za miaka 20 za kuvutia wawekezaji na kujenga uchumi shirikishi.
Alisema
kamati hiyo inahimiza wananchi kuzingatia kuwa msingi wa uchumi wetu ni
uwekezaji kutoka ndani na nje ya nchi. Msingi wa kuvutia wawekezaji ni
utawala wa sheria. Juhudi za serikali ya CCM za kuua utawala wa sheria
zitaua uwekezaji na kuangamiza uchumi wa nchi. Tusiruhusu CCM iue uchumi
wa nchi kwa maslahi yake ya kisiasa na viongozi wake.
SHARE
No comments:
Post a Comment