TRA

TRA

Thursday, September 8, 2016

Obama: Trump hana uwezo wa kuiongoza Marekani

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Rais Obama
Rais Obama amesema kuwa kila mara Bw Trump anapoongea inabainika kwazi kwamba mgombea wa Republican hafai kuwa rais
Rais Barack Obama amemtaja Donald Trump "wa ajabu" na "asiye na ufahamu" baada ya mgombea huyo wa Republican kusema kuwa rais wa Urusi Vradimir Putin ni kiongozi mzuri zaidi kuliko Obama.
Akizungumza Laos, Bw Obama amesema kuwa kila mara Bw Trump anapoongea inabainika kwazi kwamba mgombea wa Republican hafai kuwa rais.
Katika kipindi cha televisheni siku ya Jumatano, Bw Trump alimsifu Bw Putin kuwa ni "mtu mwenye uwezo mzuri wa kudhibiti mambo" na kumpa kiwango cha asilimia 82% cha uwezo huo.
Donald Trump
Bw Trump alimsifu Bw Putin kuwa ni "mtu mwenye uwezo mzuri wa kudhibiti mambo" na kumpa kiwango cha asilimia 82% cha uwezo huo
Bw Trump na hasimu wake Hillary Clinton walikuwa wakijibu maswali kutoka kwa wanajeshi wa zamani.
Rais Obama alisema: "sidhani kama ana uwezo wa kuwa rais wa Marekani na kila anapozungumza, suala hili linathibitika."
Rais huyo wa Marekani alielezea kuhusu kazi ya kidiplomasia aliyokabiliana nayo katika mikutano yote wa Asean na Laos pamoja na ule wa awali wa G20 nchini Uchina.
Alisema : "Siwezi kukuelezea yote kuhusu mazungumzo niliyokuwa nayo katika kipindi cha siku nane siku tisa zilizopita na viongozi wa kigeni kwamba hii ni kazi''.
" Unapaswa kufahamu ni nini unachokizungumza, lazima kwanza ufanye kazi ya kuelewa mambo. Unapoongea , lazima kile unachokiongea kiwe kinafanana na sera unayofikiria unaweza kuitekeleza'' Alisema Obama.BBC

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger