Meneja
mawasiliano ya ndani wa kampuni ya TBL group,Zena Tenga (wa kwanza
kulia) akisalimia na watendaji wa kituo kulelea watoto walemavu cha
Human Dream Children Village,Emanuel Komba kushoto ni mama mlezi wa
kituo hicho,Celina Fransis na kulia ni Meneja wa mawasiliano ya nje wa
kampuni hiyo Amanda Walter
Meneja
mawasiliano ya ndani wa kampuni ya TBL group,Zena Tenga (wa pili kulia)
akimkabidhi moja ya kiroba cha chupa zilizovunjika kwa ajili ya ujenzi
wa uzio Mkurugenzi msaidizi wa Kituo cha kulelea watoto walemavu cha
Human Dream Children Village,Emanuel Komba kushoto ni mama mlezi wa
kituo hicho,Celina Fransis na kulia ni Meneja wa mawasiliano ya nje wa
kampuni hiyo Amanda Walter
Mkurugenzi
msaidizi wa kituo cha kulelea watoto walemavu Human Dream Children
Village,Emanuel Komba akiwaonyesha mazingira ya kituo hiko baadhi ya
wafanyakazi wa kampuni ya TBL group kutembelea kituo hiko na kukabidhi
msaada wa vipande vya chupa vya kutengenezea uzio wa kituo hicho
Mkurugenzi
msaidizi wa kituo cha kulelea watoto walemavu Human Dream Children
Village,Emanuel Komba(kulia) akiwaonyesha mmoja wa watoto wanaolelewa
katika kituo hicho baada ya baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TBL
group kutembelea kituo hiko na kukabidhi msaada wa vipande vya chupa vya
kutengenezea uzio wa kituo hicho
Kituo cha
kuwahudumia watoto wenye ulemavu cha Human Dream Children Village
kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam, ambacho kimekuwa kikikabiliwa
na changamoto ya matukio ya wizi kimepata msaada wa vipande vya chupa
kwa ajili ya kuimarisha uzio wake kutoka kampuni ya TBL Group.
Msaada
huo kwa kituo hicho ni moja ya mkakati wa kampuni ni moja ya mkakati wa
kampuni wa kutekeleza kanuni ya afya na usalama ambayo mbali na kulenga
maeneo ya kazi inalenga pia kwa jamii kwa ujumla.
Meneja
Mawasiliano wa TBL Group,Zena Tenga,alisema kuwa moja ya sera ya kampuni
inatoa kipaumbele kutekeleza suala la Afya na Usalama kuanzia kwa
wafanyakazi ,wageni wanaotembelea viwanda vyake,wateja na jamii kwa
ujumla.
“Kutokana
na sera ya Afya na Usalama tumeguswa na tatizo la kituo hiki la
kutokuwa na usalama ndio maana tumeamua kuwaletea vipande hivi vya
chupa vya kuweka kwenye kwenye uzio kwa ajili ya kuimarisha
usalama.Vilevile moja ya mkakati wa kampuni ni kuunga mkono jitihada za
serikali za kukabiliana na changamoto mbalimbali za kijamii”.Alisema
Tenga.
Kwa
upande wake Msimamizi Msaidizi wa kituo hicho Emmanuel Komba,ameishukuru
kampuni ya TBL msaada huo ambao alidai utasaidia kuondokana na
changamoto ya matukio ya wizi na kuhatarisha usalama wa watoto wanaoishi
kituoni hapo. “Tunashukuru kwa msaada huu mkubwa kwa kuwa utasaidia
kuimarisha hali ya usalama hapa kituoni”.Alisema Komba. (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment