TRA

TRA

Wednesday, September 7, 2016

WAZIRI MKUU AKAGUA UJENZI WA MAKAZI YAKE MAPYA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


UKA1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Badhi ya Mawaziri na viongozi wa mkoa wa Dodoma baada ya kukagua ujenzi wa makazi mapya ya Waziri Mkuu kwenye kilima cha Mlimwa mjini Dodoma Septemba 7,2016. Katikati ni mkewe Mary.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
UKA2
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia  kwake ) wakikagua ujenzi wa makazi mapya ya Waziri Mkuu kwenye kilima cha Mlimwa mjini Dodoma Septemba 7, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
UKA3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia  kwake ) wakikagua ujenzi wa makazi mapya ya Waziri Mkuu kwenye kilima cha Mlimwa mjini Dodoma Septemba 7, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
UKA4
WAZ1
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa na Mkewe Mary  (kushoto)  wakipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama kuhusu ujenzi wa makazi mapya ya Waziri Mkuu, kwenye kilima cha Mlimwa mjini Dodoma Septemba 7, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZ2
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia  kwake ) wakikagua ujenzi wa makazi mapya ya Waziri Mkuu kwenye kilima cha Mlimwa mjini Dodoma Septemba 7, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa makazi mapya ya Waziri Mkuu katika eneo la Mlimwa na kuagiza umalizike kwa wakati ili aweze kuhamia kama alivyoahidi.
Katika ziara hiyo aliyoifanya leo mchana (Jumatano, Septemba 7, 2016) Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na namna kazi ya ujenzi inavyofanyika.
“Nimekuja kukagua makazi mapya na mahali pa kufanyia kazi. Kazi ya ujenzi inaendelea vizuri, nimejionea mwenyewe na naamini katika kipindi kifupi watakuwa wamekamilisha,” amesema.
Amesema kutokamilika kwa ujenzi huo hauwezi kukwamisha azma yake ya kuhamia Dodoma kwa sababu tayari inafahamika kuwa Makao Makuu ya Ofisi ya Waziri Mkuu yako Dodoma.
Amesema uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma hautokani na shinikizo la kisiasa bali ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao chimbuko lake ni agizo lililotolewa Oktoba Mosi, 1973 kwenye Mkutano Mkuu wa 16 wa chama cha TANU.
“Tangu wakati huo Serikali zote ziliendelea kufanya juhudi mbalimbali za kuandaa miundombinu na hata awamu ya nne ilisimamia kwa kiwango kikubwa uwekaji wa miundombinu hiyo,” amesema.
“Pia tukumbuke kauli ya Mheshimiwa Rais aliyotoa kwenye hotuba yake ya Julai 23, 2016 alipochaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa CCM, na akairudia tena Julai 25, kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa na mimi siku hiyo hiyo nikaweka msisitizo,” amesema.
Amesema uamuzi wa Serikali ya awamu ya tano wa kuhamia Dodoma unakuja baada ya kuridhishwa na ujenzi wa miundombinu na maeneo ya kutolea huduma za kijamii kwa wageni na wenyeji ikiwemo Hospitali ya Benjamini Mkapa iliyopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) yenye uwezo wa kutibu magonjwa makubwa kama ya moyo na figo.
Waziri Mkuu amesema tayari Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) ina mpango kamambe (master plan) na ina viwanja vya kutosha kujenga makazi na ofisi mbalimbali.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
DODOMA.
JUMATANO, SEPTEMBA 7, 2016.(P.T)

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger