Picha na Habari za Freddy
Macha, London
Balozi
wetu Uingereza, mheshimiwa Dk Asha Rose Migiro alihutubia jumuiya ya Watanzania na Waingereza (British
Tanzania Society- BTS) Jumamosi
iliyopita.
Hotuba hiyo iliyofanyika ukumbi wa Central Hall Westminster, London
ni mara ya pili kwa balozi huyu mgeni kukutana na BTS. Mwezi Julai
alikaribishwa rasmi akiwa na Balozi mpya Uingereza Tanzania Bi Sarah Cooke na
aliyestaafu, Bi Diana Melrose.
Mada
hiyo iliyoitwa “Maendeleo ya Sasa Tanzania”
Ilikuwa sehemu ya mkutano wa 41 wa mwaka wa BTS na kuhudhuriwa na
Watanzania na Waingereza wakazi hapa.
Wajumbe
wa BTS wanaipenda Tanzania na kusimamia miradi tele kwa kujitolea bila hata
senti moja. Mwaka 2015-2016 BTS imeendeleza mipango 46 ya maendeleo haya.
Mama
Balozi alizungumza kifupi akisisitiza masuala muhimu ya maendeleo ya elimu,
uongozi mpya wa Rais John Magufuli
unaosisitiza “Hapa Kazi Tu” katika kipindi cha mwaka mzima. Baada ya hapo
alitumia muda mwingi kujibu maswali ya wajumbe. Aidha masuala yalijibiwa au kupewa ahadi ya kufuatiliwa kivitendo.
Balozi wetu Uingereza, mheshimiwa Dk Asha Rose Migiro alihutubia
jumuiya ya Watanzania na Waingereza (British Tanzania Society- BTS)
Jumamosi iliyopita. Hotuba hiyo iliyofanyika ukumbi wa Central Hall
Westminster, London ni mara ya pili kwa balozi huyu mgeni kukutana na
BTS. Mwezi Julai alikaribishwa rasmi akiwa na Balozi mpya Uingereza
Tanzania Bi Sarah Cooke na aliyestaafu, Bi Diana Melrose.
Mada hiyo iliyoitwa “Maendeleo ya Sasa Tanzania” Ilikuwa sehemu ya
mkutano wa 41 wa mwaka wa BTS na kuhudhuriwa na Watanzania na Waingereza
wakazi hapa.
SHARE
No comments:
Post a Comment