Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Uwekezaji,Profesa Adolf Mkenda (kushoto) akibadilishana
mawazo na Meneja Mradi wa BEST-DIALOGUE, Bw.Hans Determeyer (katikati) wakati wa
majadiliano yaliyohusu kuongeza kasi ya ubunifu na ukuaji wa wajasiriamali kupitia sera
wezeshi zenye kutekelezeka na (kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi
(TPSF),Bw. Godfrey Simbeye. Picha na Mpiga picha wetu,Dar es Salaam.
Wadau wa masuala ya biashara wa ndani na nje ya nchi wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa
majadiliano iliyotolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Uwekezaji ,Profesa Adolf
Mkenda (hayupo pichani), wakati wa majadiliano yaliyohusu kuongeza kasi ya ubunifu na
ukuaji wa wajasiriamali kupitia sera wezeshi zenye kutekelezeka.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF),Bw. Godfrey Simbeye (kulia) akitoa
taarifa juu ya maendeleo ya sekta binafsi nchini, wakati wa majadiliano yaliyohusu kuongeza
kasi ya ubunifu na ukuaji wa wajasiriamali kupitia sera wezeshi zenye kutekelezeka, wa pili
kulia Meneja Mradi wa BEST-DIALOGUE, Bw.Hans Determeyer , katikati ni Mkurugenzi wa
Program ya Kimataifa ya SEPT,Profesa Utz Donberger, (wa pili kushoto) ni Katibu Mkuu
Wizara ya Viwanda na Uwekezaji ,Profesa Adolf Mkenda na kushoto ni Mkuu wa Kitivo cha
Biashara Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS) ,Dk. Ulingeta Mbamba.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda (kulia) akifungua
majadiliano yaliyohusu kuongeza kasi ya ubunifu na ukuaji wa wajasiriamali kupitia sera
wezeshi zenye kutekelezeka, (wa pili kulia) Meneja Mradi wa BEST-DIALOGUE, Bw.Hans
Determeyer , (katikati) ni Mkurugenzi wa Program ya Kimataifa ya SEPT, Profesa Utz
Donberger, (wa pili kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF),Bw.
Godfrey Simbeye na (kushoto) ni Mkuu wa Kitivo cha Biashara Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDBS),Dk. Ulingeta Mbamba.
SERIKALI
imeshauriwa kuweka mazingira ambayo yatasaidia kuwa na sera bora na
mifumo mizuri ya kisheria inayochangia kukuza sekta ya Ujasiriamali
(SME) ambayo pia itaongeza ajira, vipato vya wajasiriamali na taifa ili
kupunguza umasikini katika jamii.
Akizungumza
hayo jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta
Binafsi (TPSF),Bw. Godfrey Simbeye amesema kuwa serikali inahitajika
kuweka mazingira yatakayo changia kuwa na sera ambayo inayolenga kukuza
kwa haraka sekta ya wajasirimali ili kukuza ajira, vipato vya
wajasiriamali na pato la taifa na kupunguza umasikini katika jamii.
“Sera
iliyopo ya mwaka 2003 ya kuendeleza ujasiriamali inahitaji kuboreshwa
zaidi ili kwenda na wakati ili kukuza na kuimarisha maendeleo ya sekta
hii” alisema Bw. Simbeye.
Aidha
Bw. Simbeye alisema kwamba majadiliano hayo yaliwaleta wadau wa masuala
ya biashara wa ndani na nje ya nchi kama Kenya,Ghana, Uganda,
Ujerumani, Uingereza,Ethiopia, Rwanda, Uholanzi, Taasisi za Biashara,
wasomi na wajasirimali na wawakilishi kutoka UN kujadili namna ya kuwa
na sera hiyo wezeshi.
Bw.
Simbeye aliongeza kuwa Tanzania imejikiwekea mikakati ya kuelekea katika
uchumi wa viwanda, hivyo serikali itambue kukuza vipaji vya wabunifu
katika sekta ya uzalishaji na ujasiriamali wadogo na wa kati kwa kupewa
motisha ili waweze kuhamasika kuibua mawazo mapya.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Uwekezaji Prof. Adolf
Mkenda alisema kuwa sekta ya ujasirimali ina mchango mkubwa kwa taifa,
na serikali imekuwa karibu katika kuhakikisha inazidi kuimarika na
kutoa mchango mkubwa.
“Pamoja
na mchango huu wa sekta hii pia tunatambua kuna changamoto mbalimbali
ambazo kwa kushirikiana na wadau wa biashara tunaweza kuifanya sekta hii
kuimarika zaidi na kuwa na mchango mkubwa kuliko ilivyo hivi sasa,”
alisema Prof. Mkenda
Aidha
Prof. Mkenda alisema serikali imeweka mazingira ambayo yanasaidia kukuza
sekta hiyo ikiwemo taasisi zote zinazohusika na masuala ya biashara
zinafanya kazi ipasavyo kusaidia wajasiriamali wadogo na wakati kuzidi
kukua.
Prof.
Mkenda alisitiza kuwa serikali itaendelea kushishirikisha sekta hiyo ili
kuhakikisha inafanya kazi kwa karibu kwani ndio injini ya uchumi wa
nchi.
Naye
Meneja Mradi wa BEST DIALOGUE,Bw. Hans Determeyer alisema maendeleo
katika nchi yanakuja kwa sekta binafsi kuwa na nguvupamoja na kuweka
mazingira wezeshi kati ya serikali na wafanyabiashara wenyewe.
“Majadiliano
haya ni chachu kwa mataifa mbalimbali yaliyoshiriki katika kuweka
mikakati inayowezesha kufikia malengo ya kiuchumi,” na kwa kufanya hivyo
ni kusaidia kupunguza hali duni za vipato kwa wananchi na nchi kwa
ujumla” alisema Bw. Determeyer.
Kwa
upande wake Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Wakatoliki nchini Ghana,George
Kafui Agbozo alisema nchi za Afrika ili ziweze kupiga hatua kiuchumi
zinahitaji kuweka mazingira ya kukuza wajasiriamali wadogo na wakati.
“Changamoto
za ukuzaji ujasirimali kwa nchi hizi za Afrika zinafanana hivyo ukikuza
ujasiriamali kuna nafasi kubwa na kupunguza umasikini,”alisema Bw.
Agbozo.
Majadiliano
hayo yaliandaliwa na TPSF, Kituo cha Utafiti wa Sera na Utetezi
(CPRA),Chuo Kikuu cha Dar es Salam Kitivo cha Biashara (UDBS),kwa
kushirikiana na Mtandao wa Maarifa na Ubunifu Afrika (iN4iN) kwa ajili
ya kupata njia bora za kuendesha ujasiriamali nchini.
SHARE
No comments:
Post a Comment