Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia)
akikaribishwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Idara ya Polisi ambaye pia ni Naibu
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (DIGP), Abdurahman Kaniki (aliyevaa tai) kwa ajili ya kufungua
kikao cha Baraza hilo, kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini
Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili
kushoto), Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Idara ya Polisi ambaye pia ni Naibu Mkuu wa
Jeshi la Polisi Nchini (DIGP), Abdurahman Kaniki (wapili kulia), Kamishna wa Fedha wa Jeshi
hilo, Albert Nyamhanga (kushoto) na Katibu wa Baraza hilo, Merise Mwanyema wakiimba
wimbo wa Mshikamano Daima kabla ya Naibu Waziri kufungua Kikao cha Baraza hilo,
kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza
na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Idara ya Polisi (hawapo pichani) wakati alipokuwa
anatoa hotuba ya ufunguzi wa kikao cha Baraza hilo kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano
wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Masauni aliwataka wajumbe
hao kufanya kazi kwa vitendo kwa kuyatekeleza ipasavyo maazimio ya kikao hicho.
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Idara ya Polisi wakiimba wimbo wa
Mshikamano Daima kabla ya Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni kufungua Kikao cha Baraza hilo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano
wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Idara ya Polisi ambaye pia Naibu Mkuu wa Jeshi la
Polisi Nchini (DIGP), Abdurahman Kaniki akizungumza na Wajumbe wa Baraza hilo (hawapo
pichani) kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni (kulia meza kuu) kufungua Kikao cha Baraza hilo, kinachofanyika
katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni
Kamishna wa Fedha wa Jeshi hilo, Albert Nyamhanga na Mwenyekiti wa Chama cha
Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Jeshi la Polisi.
Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi Idara ya Polisi kutoka Zanzibar, Shemsa Said akichangia
mada katika kikao cha Baraza hilo kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza,
Ukonga jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akijibu
maswali ya waandishi wa habari mara baada ya kufungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi
Idara ya Polisi kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza, Ukonga jijini Dar es
Salaam. Masauni aliwaambia waandishi hao, Jeshi la Polisi linaendelea kupambana na madawa
ya kulevya pamoja na kulinda usalama wa raia na mali zao nchini ikiwa ni sehemu ya majukumu
yao. Pia aliwataka wajumbe wa Baraza hilo kufanya kazi kwa vitendo kwa kuyatekeleza
ipasavyo maazimio yote ya kikao hicho. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
SHARE
No comments:
Post a Comment