Mkurugeni
mtendaji wa GGM wa pili kulia Bw. Terry Mulpeter akimuonyesha Naibu
waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina
katikati, bwawa linalotumika kusambaza maji safi katika mji wa Geita.
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Mungano na Mazingiraa Mhe. Luhaga Mpina
akijiandaa kwenda sdehemu ya chini ya ardhi ya mgodi wa GGM
Sehemu
ya chini ya ardhi (underground) yenye dhahabu ya mgodi wa GGM
inayosemekaka kukosa huduma ya choo kwa watumishi wanaokadiriwa kuwa
zaidi ya mia tatu, ikionekana kwa nje katika katika picha.
Bw.
Simon Mushy Makamu wa Rais wa Mgodi wa GGM akijibu maswali ya Naibu
Waziri Ofisi ya Maku wa Rais Mungano na Mazingira mhe Luhaga Mpina
hayupo pichani kuhusu suala la mgodi kutiririsha maji ya mvua
yaliyochanganyikana na sumu kutoka mgoni kwenda katika mazingira na
maeneo ya vijiji jirani na Katoma
Sehemu ya kutupia na kutetekeza taka ngumu katika mgodi wa GGM Geita.
Mabwawa
Ya majitaka la Mgodi wa dhabu wa Geita wa Geita Gold Mining maarufu
kama GGM, ambapo imeelekezwa kuweka mtambo wa kusafisha Majitaka hayo
kuingia katika mabwawa.
……………………………………………………………
Na Evelyn Mkokoi, Geita
Mgodi
maarufu wa kuchimba dhahabu mjini Geita wa GGM umekumbana na adhabu ya
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC katika Ziara
ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.
Luhaga Mpina Mkoani Geita kwa kosa la kukosa vyoo vya wafanyakazi zaidi
ya mia tatu (300) katika eneo la chini ya ardhi underground la
uchimbaji wa madini ya dhahabu.
Hali hiyo imeipelekea NEMC kuutoza mgodi huo faini ya shilingi milioni 10, zinazotakiwa kulipwa ndani ya siku kumi na nne.
Katika
ziara hiyo iliyomlazimu Naibu Waziri Mpina kuvaa vifaa maluum ili
kuweza kuingia katika eneo la chini ya ardhi lenye mwamba mkubwa wa
mgodi huo, akiambatana na baadhi ya maafisa aliongozana nao katika ziara
yake, Naibu Waziri alijionea namna ambavyo eneo lenye idadi kuwa ya
wafanyakazi kukosa huduma hiyo muhimu ya choo inayowapelekea kujisaidi
vichakani na kuharibu mazingira.
Aidha
Naibu Waziri Mpina Pia aliweza kujionea uharibifu mwingine unaofanywa na
mgodi huo wa utiririshwaji wa Maji ya mvua yaliyochanganyikana na
madawa hatarishi kwa mazingira na viumbe hai kwenda kwenye makazi ya
wananchi.
Kufuatia
hali hiyo, Naibu waziri Mpina alielekeza uongozi wa mgodi huo kujenga
miundombinu rafiki kwa mazingira yatakayopelekea maji hayo kwenda katika
mkondo sahihi..
Akiongea
kwa Niaba ya GGM makamu wa Rais wa Mgodi huo Bw. Simon Mushy, alisema
kuwa wapo kwenye mchakato wa kujenga miundombinu kwa kushiriana na
Halmashauri ya Mji wa Geita.
Kwa
upande wa mmoja wa wakazi wa kijiji cha Katoma Bi. Magori James Katoka
alisema kuwa vumbi na maji ya mvua vinavyotoka kwenye mgodi huo
vimekuwa ni kero na changamoto ya muda mrefu katikma kijiji hicho.
Pamoja
na malalamiko mengi ya wakazi wa Katoma Geita kuhusu uharibifu wa
mazingira unaofanywa na mgodi wa GGM, Mgodi huo pia umefanya shughuli
mbali mbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kusambaza maji safi a salama
katika mji wa Geita ukishirikiana na mamlaka ya maji safi na maji taka
ya Mkoa huo.
Ziara
ya Naibu Waziri Mpina Katika Mkoa wa Geita ni muendelezo wa ziara yake
ya ukaguzi wa mazingira katika viwanda na migodi nchini.
SHARE
No comments:
Post a Comment