Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya ileje Haji Mnasi akiwa kwenye eneo husika la kukagua wakwepa kodi.
Hawa ni baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wialaya ya Ileje wakifutalia jambo lililokuwa likiongelewa na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya ileje haji mnasi
Hili ni moja ya malori yaliyokuwa yakikwepa ushuru kwa kufanya biashara ya kushusha mizigo vichochoroni.
Hili
ni moja kati ya gari linalobeba milunda bila kulipia ushuru na
mkurugenzi Haji Mnasi kufanikiwa kulikamata wakati wa zoezi maalumu la
kuwatafuta wakwepa kodi waliobobea kuikimbia serikali kulipa kodi
Na Daniel Mwambene, Songwe
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje wampongeza
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Haji Mnasi kwa kukuza uchumi wa wilaya
hiyo na kufanikiwa kuwadhibiti wafanyabiashara waliokuwa wakikwepa kodi.
Pongezi
hizo zilitolewa na madiwani hivi karibuni wakati wa kikao cha Kamati ya
Fedha,Uongozi na Mipango kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri.
Akizungumza na blog hii diwani wa kata ya Itumba Mohamed Mwalaalisema
kuwa wanatambua juhudi zilizofanywa na Mkurugenzi Haj Mnasi na
wafanyakazi wa halmashauri kukusanya ushuru maeneo mbalimbali na
kufanikiwa kuyakamata magari aina ya maroli yaliyokuwa yakikwepa ushuru.
Naye diwani wa kata ya Ibaba Tata Kibona alisema kuwa mkurugenzi na timu yake wamekuwa wakitembea usiku kuwatafuta wakwepa kodi hasa kwenye kata yake ambapo mara kadhaa mkurugenzi huyo amekuwa akionekana nyakati za usiku.
"mimi sijawahi ona mkurugenzi kama huyu maana anaacha usingizi wake unamkuta kwenye kata nyakati za usiku akipambana nao wakwepa kodi na amefanikiwa kuwadhibiti wafanyabiashara wote wakwepa kodi na ndio maana sasa mapato yameanza kukua kwa kasi katika wilaya yetu"alisema Kibona
Naye diwani wa kata ya Ibaba Tata Kibona alisema kuwa mkurugenzi na timu yake wamekuwa wakitembea usiku kuwatafuta wakwepa kodi hasa kwenye kata yake ambapo mara kadhaa mkurugenzi huyo amekuwa akionekana nyakati za usiku.
"mimi sijawahi ona mkurugenzi kama huyu maana anaacha usingizi wake unamkuta kwenye kata nyakati za usiku akipambana nao wakwepa kodi na amefanikiwa kuwadhibiti wafanyabiashara wote wakwepa kodi na ndio maana sasa mapato yameanza kukua kwa kasi katika wilaya yetu"alisema Kibona
Akielezea
mafanikio hayo Mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Godfrey
Zimubiha alisema kuwa mafanikio hayo yanachangiwa na wadau mbalimbali
ukiwemo uongozi ngazi ya wilaya,kata vijiji na wananchi kwa ujumla.
Kwa
upande wake mkurugenzi wa Halmahauri hiyo Haji Mnasi aliwapongeza
wananchi,watumishi wa ngazi zote za wilaya na madiwani wote kwa kufanya
kazi kwa weledi wao na kufanikisha malengo ya wilaya hiyo hata hivyo
alimshukuru mkuu wa wilaya ya Ileje Joseph Mkude kwa ushirikiano
anaoutoa
“Nashukuru
mungu sasa madiwani wa wilaya yangu wameacha siasa na wanafanya kazi
kwa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe
Magufuri kwa kile anachokifanya kuleta maendeleo ya nchi yetu na ndio
maana unaona hata huku kwetu pato letu la wilaya limekuwa”alisema Mnasi
Aidha
Mh Mnasi aliyataja baadhi ya maeneo yaliyokuwa korofi wakati wa ulipaji
wa ushuru ni kama kata ya Ngulilo ambako kulikuwa na utoroshaji wa
mazao ya mbao pamoja na kata ya Mbebe na Isongole ambako nako kulikuwa
na utoroshaji wa nafaka.
Mnasi
aliwaonya wafanyabiashara wanaokwepa ushuru au kodi kwa kuwa zoezi hilo
litakuwa endelevu na elimu itaendelea kutolewa kuanzia ngazi ya
kitongoji hadi wilaya ili kuwabaini wakwepaji wa ushuru ambao wanaathiri
maendeleo ya wilaya hiyo.
“Nasema
kuwa nitakula nao sahani moja wafanyabiashara wote wanakwepa ushuru
hadi pale watakapo acha tabia hiyo na kusaidia uchumi wa halmashauri ya
wilaya ya Ileje kukua kwa kasi inayostahili”alisema Mnasi
Wilaya ya Ileje hutegemewa sana kwa uzalishaji wa mbao ambazo husafirishwa kwenda katika mkoa wa Songwe na Mbeya.
SHARE
No comments:
Post a Comment