Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na
washiriki wa mashindano ya SHIMMUTA wakati wa uzinduzi wa mashindano
hayo Novemba 24, 2016 yanayofanyika Jijini Tanga.
Baadhi ya Timu zikiwasili katika katika Uwanja wa Mkwakwani kwa ajili ya mashindano ya SHIMMUTA yanayofanyika Jijini Tanga.
Baadhi ya Timu zikiwasili katika katika Uwanja wa Mkwakwani kwa ajili ya mashindano ya SHIMMUTA yanayofanyika Jijini Tanga.
Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye na Mwenyekiti
wa SHIMMUTA Bw. Hamis Mkalachi wakipokea maandamano ya timu shiriki
zilizopokuwa zikiwasili katika Uwanja wa Mkwakwani kwa ajili ya
mashindano ya SHIMMUTA yanayofanyika Jijini Tanga.
Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akicheza
muziki aina ya kwaito pamoja na wachezaji na viongozi wa timu shiriki
wakati wa sherehe za uzinduzi wa mashindano ya SHIMMUTA yanayofanyika
Jijini Tanga.
Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikagua timu
mbalimbali kabla ya kuanza kwa michezo mbalimbali wakati wa uzinduzi wa
mashindano ya SHIMMUTA yanayofanyika Jijini Tanga.
Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikagua timu
mbalimbali kabla ya kuanza kwa michezo mbalimbali wakati wa uzinduzi wa
mashindano ya SHIMMUTA yanayofanyika Jijini Tanga.
Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipiga mpira
kuashiria uzinduzi rasmi wa mashindano ya SHIMMUTA yanayofanyika Jijini
Tanga.
Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akionesha
ufundi wa kupiga danadana wakati wa uzinduzi rasmi wa wa mashindano ya
SHIMMUTA yanayofanyika Jijini Tanga, akimshuhudia akipiga danadana hizo
ni Mbunge wa Tanga Mjini Mhe.Musa Mbaruk.Picha zote na Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini WHUSM.
Na Mwandishi Wetu- Tanga.
Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amekemea vikali
baadhi ya tabia ya viongozi wa timu zinazoshiriki michezo mbalimbali
kutumia wachezaji wasiostahili kutumika katika mashindano husika.
Ameyasema
hayo wakati akizindua mashindano ya michezo mbalimbali yanayoandaliwa na
Shirikisho la Michezo ya mashirika ya Umma na Binafsi (SHIMMUTA)
yanayoendelea Jijini Tanga ambayo yameshirikisha timu mbalimbali kutoka
mashirika ya Umma na Binafsi Tanzania.
Mhe. Nnauye
amewataka viongozi wa SHIMMUTA kufanya uhakiki upya wa wachezaji wa timu
shiriki ili kuondoa lawama zinazoweza kutokea na kupata mshindi
anayestahili kwa kufata Sheria na taratibu zote za mashindano.“Nawaomba
viongozi muangalie na kupitia upya wachezaji wa timu shiriki ili kusiwe
na zengwe lolote katika mashindano haya na mshindi katika kila mchezo
apatikane kihalali” alisisitiza Mhe. Nnauye.
Aidha ametoa
wito kwa mashirika kutenga muda na fedha ili kuwezesha timu zao
kushiriki katika michezo ikiwa ni moja ya kujenga mshikamano na amani
kwa watanzania na pia kujenga afya ya mwili na akili.Mashindano
ya SHIMMUTA yameshirikisha mashirika ya Umma na Binafsi katika michezo
12 ikiwemo Mpira wa Miguu(Football), Mpira wa Pete(Netball),kuvuta
kamba, Riadha, Mchezo wa vishale(Darts),Mchezo wa Pooltable, mchezo wa
bao, Karata,kukimbia na magunia.
SHARE
No comments:
Post a Comment