Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi
Mramba, (katikati), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam, leo Novemba 24, 2016. Alikuwa akitoa ufafanuazi
kuhusu masuala muhimu ya TANESCO. Wengine pichani, kulia ni Meneja wa
Vyuo vya TANESCO, Mhandisi Said Msemo na kushoto ni Kaimu Meneja Uhisano
wa Shirika hilo, Leila Muhaji.
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
SERIKALI
kupitia Shirika lake la umeme nchini TANESCO limefanya uwekezaji mkubwa
kwenye miradi mbalimbali ya umeme yenye thamani ya Shilingi Trilioni
5.35, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Mhandisi Felchesmi Mramba
amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Novemba 24,
2016.
Akitoa
ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali muhimu ya Shirika hilo, Mhandisi
Mramba alisema, “Katika historia ya sekta ya umeme, haijawahi kutokea
uwekezaji mkubwa kufanyika kwa wakati mmoja kama ilivyo sasa, Miradi
yote ya umeme inayoendelea na ambayo tayari iemtengewa fedha ina thamani
ya Shilingi Trilioni 3.85, na majadiliano kati ya Serikali na Exim Bank
ya mradi wa Dar es Salaam-Arusha wa Shilingi Trilioni 1.5 yakiwa katika
hatua za mwisho.” Alifafanua Mhandisi Mramba.
Uwekezaji
huu unathibitisha kwamba nia ya Serikali ya awamau ya tano ya kuifanya
Tanzania kuwa nchi ya viwanda sio ya maneno matupu bali inaambatana na
vitendo kwa uwekezaji madhubuti kwenye umeme.” Alisema.
Mhandisi
Mramba alitaja Miradi hiyo mikubwa ya umeme kuwa ni pamoja na ule wa
upanuzi wa Kinyerezi I, Kinyerezi II, mradi wa Backbone, Kenya-Tanzania,
TEDAP, Makambako-Songea, Uboreshaji umeme jijini Dar es Salaam, City
Centre-Dar es Salaam, Electricity V, Bulyanhulu-Geita, Geita Nyakanazi
na Rusumo Power Plant
(T), miradi yote hii ikiwa na jumla ya thamani ya Shilingi Trilioni 3.85.
(T), miradi yote hii ikiwa na jumla ya thamani ya Shilingi Trilioni 3.85.
Akifafanua
zaidi kuhusu uwekezji huo, Mhandisi Mramba alisema, Miradi yote ambayo
thamani yake imetajwa haihusishi Miradi ya usambazaji umeme Vijijini
chini ya mpango wa REA.
Akizungumzia
utaratibu mpya wa manunuzi,(Procumbent), Mhandisi Mramba alisema,
TANESCO imechukua hatua kadhaa ili kuboresha manunuzi ambapo kuanzia
sasa makampuni yanayomilikiwa na mtu mmoja kuhodhi manunuzi ya Shirika
hilo, na kwamba zabuni zote zilizotangazwa kuanzia mwaka huu wa fedha,
haitaruhusiwa kampuni moja kuwa na mikataba miwili kwa wakati mmoja.
Akifafanua
zaidi alisema, Katika zabuni moja haitaruhusiwa kampuni moja kupewa
zaidi ya Lot 1, “Hii imeanza kusaidia kuondoa ukiritimba katika manunuzi
na kuwapa Watanzania wengi zaidi nafasi pana ya kushiriki katika zabuni
za kusambaza vifaa vya umeme.” Alifafanua Mhandisi Mramba.
Aidha
Mhandisi Mramba alisema, ili kuwezesha Watanzania wengi kushiriki katika
uchumi wa nchi, TANESCO itanunua vifaa vya umeme vinavyozalishwa hapa
nchini na kuachana na mtindo wa kuagiza kutoka nje.
“Mfano
kwa nguzo za umeme tumewapa Sao Hill, ambao watatuuzia nguzo 96,500, na
new Forest watatuuzia nguzo za umeme 9,668, na kwa upande wa Transfoma
za umeme, kandarasi hiyo imepewa kampuni ya TANELEC itakayotuuzia
transfoma 1,500” Alifafanua
Akieleza
zaidi kuhusu ununuzi wa vifaa, Mhandisi Mramba alisema, kampuni ya East
Africa Cables, intarajiwa kupewa kazi ya kusambaza waya na kuongeza kuwa
utaratibu huo pia utatumika kwenye huduma nyingine kama vile Bima,
ambapo alisema Shirika linatarajia kulitumia Shirika la Bima la Taifa,
(NIC), kutoa huduma hiyo.
Akizungumzia
kuhusu hali ya umeme, Mhandisi Mramba aliwahakikishia Watanzania kuwa
kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Shirika hilo katika kuboresha
miundombinu ya umeme, hakutakuwa na mgao wa umeme nchini na ndio maana
kwa muda mrefu sasa hakuna mgao wa umeme.“Mwaka 2015 nchi ilikuwa na
mgao wa umeme wa jumla ya MW300, na maeneo mengine yalikuwa na hali
mbaya hususan Mwanza, Arusha na Kilimanjarolakini
kwa sasa hali ya umeme katika mikoa yote na mingine ni nzuri hakuna mgao na kama ikitokea umeme umekatika ni matatizo ya kiufundi katika eneo dogo na kwa muda mfupi.” Alisema.
kwa sasa hali ya umeme katika mikoa yote na mingine ni nzuri hakuna mgao na kama ikitokea umeme umekatika ni matatizo ya kiufundi katika eneo dogo na kwa muda mfupi.” Alisema.
Hata
hivyo alisema Shirika lake linaongeza juhudi za kusambaza umeme kwa
watanzania wengi zaidi kote nchini, kutokana na uwekezaji wa miundombinu
unaoendela kila kona ya nchi.
Mhandisi
Mramba aliwaondoa wasiwasi wananchi kuhusu ombi la Shirika hilo la
kuongeza asilimia 18.9 ya bei ya umeme kuanzia Januari mwakani, kwa
kusema ongezeko hilo halitaathiri watumiji wa kawaida majumbani.
“Tunachoomba kutoka kwa Msimamizi (Regulator), ni kufanya mabadiliko ya
kutenganisha watumiaji umeme wa majumbani na wale wanaotumia kibiashara
kama vile mabango ya matangazo, kwani hivi sasa wote wanalipa gharama
sawa na hili si sawa.” Alisema.
Aliwaasa
wananchi kuridhia ongezeko hilo kwani Shirika limo katika jitihada kubwa
za kuhakikisha Wananchi wengi zaidi wanapatiwa umeme kwa kufikisha
miundombinu ya umeme kwenye maeneo mbalimbali ya nchi, ambapo gharama za
kufanya hivyo zimeongezeka.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji, (kushoto), akizunguzma jambo
SHARE
No comments:
Post a Comment